Mkurugenzi
Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano
la kimataifa la madaktari bingwa wa mifupa linalofanyika Tanzania (MOI) Kuanzia
tarehe 26 -30 May 2019 katika ukumbi mpya wa mikutano MOI.
Madaktari
wa Mifupa kutoka mataifa mbalimbali wakifuatilia mada katika kongamano la
kimataifa linalofanyika MOI.
Madaktari
wa Mifupa kutoka mataifa mbalimbali wakifuatilia mada katika kongamano la
kimataifa linalofanyika MOI
Mkurugenzi
Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza na waandishi wa Habari
(Hawapo pichani) katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa mifupa
linalofanyika Tanzania (MOI) Kuanzia tarehe 26 -30 May 2019 katika ukumbi mpya
wa mikutano MOI
Mratibu
wa Kongamano la Kimataifa la madaktari Bingwa wa Mifupa Dkt Joseph Mwanga
akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa kongamano hilo.
Dar es Salaam, Tanzania
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dkt Respicious Boniface leo amefungua
kongamano la kimataifa la madaktari wa Mifupa linalofanyika kwa siku tano hapa
Tanzania ambapo madaktari zaidi ya 150 kutoka mataifa ya Afrika na sehemu
mbalimbali duniani wanashiriki.
Dkt Boniface amesema Kongamano hilo limekua
likifanyika hapa nchini kila mwaka kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwapa
mbinu mpya za matibabu ya mifupa madaktari hapa nchini na nchi nyingine barani
Afrika kutokana na MOI kuwa kituo cha mafunzo kutokana na huduma bora za mifupa
inazotozitoa.
“Madaktari bingwa wetu hapa nchini wamekua wakinufaika
sana na kongamano hili, wamekua wakipewa mbinu mpya na zakisasa za matibabu na
upasuaji wa mifupa jambo ambalo limepelekea MOI kuweza kumaliza rufaa za nje ya
nchi kwa wagonjwa wa mifupa ambapo kwa sasa huduma karibia zote zinapatikana
hapa nchini” Alisema Dkt Boniface.
Mratibu wa Kongamano hilo Dkt Joseph Mwanga amesema
mafunzo yatatolewa kwa njia ya nadharia, vitendo katika chumba cha maabara kwa
kutumia mifupa bandia na kwenda kwenye chumba maalum cha kujifunzia kwa kutumia
miili ya binadamu (Cadavers).
“Kongamano hili limekua na manufaa makubwa sana kwetu,
tumekuwa tukipata mbinu mpya kila mwaka kutoka kwa wenzetu wa Marekani jambo
ambalo limefanya huduma za mifupa hapa nchini ziendelee kuwa bora ukilinganisha
na mataifa mengine barani Afrika” Alisema Dkt Mwanga.
Kwa upande wake Profesa Michael Terry ambaye ni
mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Calfonia cha San Francisco amesema ushirikiano
kati ya Taasisi yake na MOI umejikita katika mafunzo ya namna ya kuwahudumia
majeruhi wa ajali kwa lengo la kuwapa huduma bora na za kisasa kwa wakati.
Kongamano hilo limeratibiwa na Taasisi ya MOI kwa
kushirikiana na Taasisi za IGOT, SIGN, OTA, AO Alliance na Chuo kikuu cha
Calfonia San Fransisco Marekani.
No comments:
Post a Comment