Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw.Nicholas William akifungua mafunzo kuhusu
Manunuzi ya Umma yanayoendeshwa na Bodi ya
Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi Tanzania (PSPTB) kwa Wakuu wa Idara na
Vitengo wa Wizara hiyo kuanzia Mei 27 -28 Jijini Dodoma. Kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu
wa Ununuzi na Ugavi Tanzania Bw.Godfrey Mbanyi na Kushoto ni Mkurugenzi Idara
ya Utawala na Rasiliamali Watu wa Wizara hiyo Bw.Orest Mushi.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Bw.Nicholas William (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi Tanzania
(PSPTB) Bw.Godfrey Mbanyi (wa pili kushoto) na Wakuu
wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo baada ya
kufungua mafunzo kuhusu Sheria ya Manunuzi ya Umma yanayoendeshwa na
Bodi hiyo kuanzia Mei 27 -28,2019 Jijini Dodoma.
Na
Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Nicholas
William amesema kuwa mafunzo ya ununuzi wa umma kwa Wakuu wa Idara na Vitengo
yatasaidia kuondoa utata uliopo kuhusu suala la kusimamia mikataba ya ununuzi
wa umma kati ya Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na
Ugavi.
Mafunzo
hayo ya siku mbili yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo pamoja na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).
“Kumekua
na utata kuhusu suala la yupi mwenye mamlaka ya kusimamia mikataba ya ununuzi
wa umma kati ya Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi hivyo
natoa rai kwa watoa mafunzo kuondoa utata huo,”alisema Bw. William.
Ameongeza
kuwa mafunzo hayo ni muhimu na yanahitajika hasa kwa viongozi wa umma kwani
ndio wahusika wakuu katika kupitisha mikataba mbalimbali ya ununuzi.
Aidha,
amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kupunguza muda unaotumika kufanya ukaguzi
kwa kuwa mikataba ya ununuzi wa umma haitakuwa na changamoto nyingi kwani
wahusika watakuwa na uelewa mpana katika maandalizi ya mikataba hiyo.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi,
Bw. Godfrey Mbanyi amesema kuwa lengo la kufanya mafunzo hayo ni kuwafanya
wanaohusika na kutoa maamuzi juu ya manunuzi ya umma kuwa na uelewa wa pamoja ili
kuhakikisha mikataba wanayoingia haileti kasoro yoyote.
“Kumekua
na changamoto kwa wakuu hawa wanapoteuliwa kuwa Wajumbe wa Bodi za Zabuni wanakuwa
hawajui chochote kuhusu taratibu za ununuzi wa umma hivyo semina hii itawasaidia
kufahamu taratibu hizo,” alisema Bw. Mbanyi.
Bw.
Mbanyi ameongeza kuwa kutokujua taratibu za manunuzi ya umma zinawasababishia
matatizo viongozi wa juu kwani vitu visiponunuliwa kwa wakati au visipokuwa na
ubora hatua zikianza kuchukuliwa zinaanzia kwa viongozi hao hivyo tukiwa na
uelewa wa pamoja utasaidia viongozi wetu wasiwajibishwe.
Vile
vile Bw. Mbanyi amefafanua kuwa Wakuu wa Idara na Vitengo wana wajibu mkubwa
kuhakikisha kwamba taratibu za manunuzi ya umma na thamani ya fedha katika
michakato wa manunuzi hayo inapatikana kwani si lengo la Serikali kupata bidhaa
na huduma kwa fedha ambazo hazina thamani halisi.
Hata
hivyo Bw. Mbanyi ametoa rai kwa waajiri kuhakikisha wanaohusika na manunuzi ya
umma katika ofisi zao wawe wamesajiliwa na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi
kwani kutokufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment