Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Walemavu Stella Ikupa, akizungumza leo na
wachezaji wa timu ya mpira wa miguu Walemavu pichani hawapo, kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu ya Watu Wenye Ulemavu
Tanzania (TAFF), Riziki Lulida na Kulia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la
Walemavu Afrika Mashariki (CECAAF), Nuru Awadhi.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Walemavu Stella Ikupa akizungumza na
wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya walemavu leo jijini Dar es
Salaam.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu wa watu wenye ulemavu wakiwa katika
mazoezi ya maandalizi ya kujiandaa na mashindano ya Afrika Mashariki
yanayotarajiwa kufanyika Juni 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI
imesema itatoa ushirikiano wa kila aina kwa timu ya mpira wa miguu kwa
watu wenye ulemavu (Tembo Worries) katika mashindano yatakayoshirikisha
nchi za Afrika Mashariki.
Hayo
yameswa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Walemavu, Stella
Ikupa wakati akizungumza na viongozi na wachezaji wa timu hiyo katika
Ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri Ikupa alisema Serikali itashirikisha wadau wote pamoja na
wabunge ili kuhakikisha mahitaji yote muhimu yanakuwepo kwa timu hiyo.
Alisema
wabunge wameanza kwa kukubali kuchangia Shilingi 100,000 sawa na
shilingi milioni 40 huku wakiendelea kushirikisha wadau wengine.
"Ninawahakikishia serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha mnachukua kombe hilo naomba msituangushe," alisema.
Alisema
awali walikuwa hawaamini kuwa kuna uwezekano wa watu wenye ulemavu
kucheza mpira wa kiwango hicho ila amejionea mwenyewe na kwamba atawapa
ushirikiano.
Ikupa alisema katika kuonesha Serikali imedhamiria kukuza michezo ofisi ya Waziri Mkuu itatoa seti tano za
fimbo za kuchezea na baiskeli ya walemavu moja ili ziweze kusaidia katika mashindano.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu
nchini (TAFF), Rizik Lulida alisema anaishukuru serikali na Spika wa
Bunge kukubali kila mbunge kuchangia mashindano hayo.
Lulida
ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Wananchi (CUF)
alisema pia TAFF inawaomba wadau mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Hifadhi
Tanzania (TANAPA) na Ngorongoro kufadhili mashindano hayo.
"Tumetumia
nembo tembo kama jina la timu tukiamini tutawalinda, kuwatangaza
wanyama wetu na kuhifadhi vivutio vyetu," alisema Lulida.
Mwenyekiti
wa Shirikisho la Michezo kwa Watu Wenye Afrika Mashariki kwa Waawake na
Watoto (CECAAF), Nuru Awadhi alisema mashindano hayo ni muhimu katika
kutangaza nchi kimataifa.
Awadhi alisema Tembo Worries, watafanya vizuri katika mashindano hayo na kuipongeza serikali kuunga mkono mchezo huo.
Rais wa TAFF, Peter Sarungi, alisema kwa sasa wana program tatu ambazo zipo mbele yao kuhakikisha wanaibuka washindi.
"Program
ya kuingia kambini, mafunzo ya marefa na mkakati wa ushindi hivyo ni
imani yangu tukifanikisha haya kila kitu kitaenda sawa," alisema.
Katika
wa CECAAF, Moses Mabula alisema alisema shirikisho limejipanga vizuri
kusimamia mashindano hayo na kwamba itapendeza kombe likibaki nyumbani.
Kwa upande wake Mchezaji Athuman Lubandani alisema wamejiandaa vizuri kuibuka na ushindi katika mash kinda hayo.
"Tunakushuru Mheshimiwa Naibu Waziri na Mama Lulida kwa mchango mnaotupatia hatutawaangusha," alisema
No comments:
Post a Comment