Madiwani
wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Songwe
Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela (hayupo pichani), katika kikao ambapo
walitoa malalamiko ya kutoridhishwa na utendaji wa Mkurugenzi wa
halmashauri ya Ileje.
Mkuu
wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela (katikati)
akiwasikiliza madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje (hawapo
pichani) katika kikao ambapo walitoa malalamiko ya kutoridhishwa na
utendaji wa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Kulia kwake ni Katibuwa CCM
Mkoa wa Songwe Mercy Mollel na Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Ileje Ubatizo Songa.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu
wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela ameunda timu ya
kuchunguza tuhuma 13 zilizo elekezwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje na
kuelekeza kuwa timu hiyo ifanye uchunguzi huo kwa haraka.
Brig.
Jen. (Mst) Mwangela amefikia uamuzi huo mara baada ya majadiliano ya kikao cha
pamoja na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje waliomuandikia barua wakiwasilisha
tuhuma za kutoridhishwa na utendaji wa Mkurugenzi huyo.
“Nimefanya
ziara Wilaya ya Ileje baada ya kupata barua kutoka kwa Madiwani wakimtuhumu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje, kabla ya kufanya maamuzi tumejadiliana na
nimefikia uamuzi wa kuunda tume ambayo itachunguza tuhuma zote 13
walizowasilisha”, ameeleza Brig. Jen. (Mst) Mwangela.
Amesema
kazi kubwa ya tume hiyo ni kuhakikisha wanapata ukweli na uhalisia juu ya
tuhuma hizo huku akielezea kuwa moja ya tuhuma ni udhaifu katika kukusanya
mapato.
“Kuna
tuhuma ambazo tunaona zina ukweli mfano Ileje haijafanya vema katika suala la
ukusanyaji wa mapato, sasa tumebakiza mwezi mmoja mwaka wa fedha uishe lakini
wamefikia asilimia 58 tu ya makusanyo ambapo ni asilimia ndogo ikiwa lengo ni
angalau zaidi ya asilimia 80 kwahiyo hapo kuna dalili za uvujishaji wa mapato”,
amefafanua Brig. Jen. (Mst) Mwangela
Brig.
Jen. (Mst) Mwangela ameongeza kuwa licha ya kwamba uchunguzi unaendelea ametoa maelekezo
na mikakati ambayo itasaidia kuhakikisha kazi ya ukusanyaji wa mapato
inaendelea vizuri.
“Lengo
ni kukusanya vizuri kwahiyo katika kikao tumeweka mikakati itakayosaidia
kukusanya mapato na tuna amini waendaji wote wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje watafanya
kazi kwa umakini mkubwa huku kamati ya fedha na mipango ya madiwani itasimamia
hilo vema”, amesema Brig. Jen. (Mst) Mwangela.
Baadhi ya tuhuma ambazo Madiwani wamezielekeza
kwa Mkurugenzi wa halmashauri ni pamoja na matumizi mabaya ya ofisi na tuhuma
katika masuala ya nidhamu
No comments:
Post a Comment