HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 24, 2019

SIMULIZI YA MAMA KUMTAFUTA MTOTO WAKE KWA MIAKA 20

Martha Kifunda.

“JINA langu naitwa Martha Kifunda (pichani), mkazi wa Tanga lakini kwa sasa nipo Kibaha mkoani Pwani kwa ndugu zangu, nimekuwa nikimtafuta mwanangu huu mwaka wa 20 sasa,” hivyo ndivyo anavyoanza kusimulia mama huyo ambaye kiumri kidogo amesogea.

Endelea kusoma simulizi yake hii ya kusikitisha akielezea jinsi ambavyo amekuwa akiteseka kumtafuta mwanaye:

“Mawazo ya kumpoteza mwanangu yamesababisha hadi kuanza kupata ugonjwa wa kupooza upande mmoja. Mwanagu Robert Gerard Kiama Pius aliondoka nyumbani mwaka 1999.


“Hadi leo naikumbuka siku ya mwisho aliyoniaga, tulikuwa tukiishi Tanga, naomba nimwambie mwanangu popote alipo, mimi mama yake namtafuta, kama ameshakufa basi nataka nijue tu ili nafsi yangu itulie.

“Alipohitimu Kidato cha Nne Shule ya Kwemvumo ipo Mombo, aliondoka na kwenda kumtafuta baba yake ambaye mara ya mwisho nilisikia alikuwa Magu mkoani Mwanza akiwa ni mwalimu katika Shule ya Nasa.

“Alirejea baada ya kumkosa. Tukaendelea kuishi kama kawaida, kutokana na maisha kuwa magumu kuna siku aliniaga kuwa anakwenda Dar es Salaam kutafuta maisha.

“Mwaka 1999, alisafiri hadi Dar na kufikia kwa ndugu zangu hawa (anaoishi nao sasa) wakati huo walikuwa wakiishi Kiwalani, akakaa hapo kwa siku mbili, baadaye aliaga kuwa anakwenda kutafuta maisha, tangu hapo hatujawahi kumuona tena.

“Jina lake kamili ni Robert Gerard Kiama Pius lakini kuna wakati alikuwa akitumia jina la Robert Kifunda, hilo Kifunda ni jina la kwetu upande wa mama. Aliamua kwenda kumtafuta baba yake mara ya kwanza ili amsomeshe kwa kuwa mimi nilikuwa sina uwezo huo kwa alipokuwa amefikia.

“Baba yake anaitwa Pius Pascal Hung’wani Shilungu, naye sijui alipo kwa kuwa tulipotezana miaka mingi na wala sina taarifa za ndugu wala rafiki yake yeyote.

“Robert ni mtoto wangu wa kwanza, mdogo wake yupo anaitwa Rogercy.

“Huu ni mwaka wa 20, sijakata tamaa, Mungu ni mkubwa naamini nitampata, naomba msaada kwa yeyote anayefahamu awasiliane na mimi au familia yangu.

“Namba yangu ni 0717 948519, namba za ndugu zangu ambazo pia wanaweza kuwasiliana nazo ni 0715 795465, 0658 764141 au 0714 899393.”

No comments:

Post a Comment

Pages