Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amehudhuria sherehe za kumwapishwa Rais wa Malawi,
Profesa, Arthur Peter Mutharika zilizofanyika jijini Blantyre.
Amehudhuria
sherehe hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa Kamuzi, Blantyre. leo
(Ijumaa, Mei 31, 2019) kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.
Akizungumza
baada kuapishwa, Rais Mutharika aliwaahidi wananchi wa Malawi kuwa
atawatumikia bila ubaguzi wa itikadi za kisiasa, kidini au ukabila.
Pia
alisisitiza kuwa hatavumilia kuona vyama vya siasa, madhehebu ya
dini au mtu yeyoye anaanzisha vurugu kwa nia ya kuikwamisha Serikali.
Rais
Mutharika alisema kuwa waliomchagua na wasiomchagua wote ni rafiki zake
na amedhamiria kuwatumikia kwa moyo wa upendo na haki.
“Uchaguzi
umekwisha mshindi amepatikana, hivyo mnapaswa kuiunga mkoano serikali
iliyodhamiria kuwaletea maendeleo wananchi wa Malawi.”
Alisema
wananchi wa Malawi wameamua kumchagua Profesa Mutharika na Chama cha
Democratic Progressive Party (DPP) hivyo lazima waheshimiwe.
Awali,
Waziri Mkuu alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chileka
alipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Malawi, Ben
Botolo.
Viongozi
wengine waliokuwepo uwanjani hapo ni pamoja na Balozi wa Tanzani nchini
Malawi, Ben Mashiba na Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Chembe
Muntali.
Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Rais Mstaafu wa Malawi, Bakili Muluzi. Mheshimiwa Majaliwa amerejea nchini leo jioni.
No comments:
Post a Comment