Kocha Mkuu wa timu ya taifa Taifa Stars, amesema wana imani kubwa
ya kuweza kuibuka na ushindi katika mchezo wa ufunguzi wao dhidi ya
Senegal, ambao ni mchezo wa kwanza utakaofanyika, Juni 23 katika Uwanja wa 30
June, Cairo,Misri.
Amunike amesema mpaka sasa wameweza kujiandaa kimbinu na
kiakili katika mchezo huo ambao anatambua wanacheza na timu kubwa Barani
Afrika, lakini hawana wasiwasi kutokana na maandalizi waliyoyafanya.
“Kikubwa katika mchezo huo,tumejiandaa kisaikolojia na
kimbinu ili tuweze kuhakikisha tunapata matokeo mazuri na tunaamini kesho
utakuwa mchezo mzuri wa mashindano,na naamini wachezaji wangu wapo kamili
kuweza kucheza mchezo huo na wanajua umuhimu wa mchezo huo.
Kwa upande wa nahodha wa Taifa Stars,Mbwana Samatta,alisema
Kwamba wanawaheshimu Senegal kwakuwa ni timu kubwa Afrika ,lakini hawatokwenda
uwanjani kinyonge.
“Kikubwa ni kwamba tutakwenda uwanjani,huku tukijua tunaenda
kupambana na timu kubwa na lazima tupambane uwanjani ili tuwezee kulisogeze
jina la nchi yetu,hivyo tunaamini kabla ya filimbi ya mwisho kila timu ina
nafasi.”
Wakati huohuo baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,wakiongozwa na Spika Job Ndugai, leo wameitembelea kambi ya timu ya
taifa Taifa Stars,iliyopo nchini Misri,inayojiandaa na mashindano ya Mataifa
Afrika.
Wabunge hao wamepata nafasi ya kuzungumza na wachezaji
pamoja na viongozi waliopo na kambi hiyo nchini Misri,kwa leongo la kuweza kuwapa
hamsa katika kuelekea mchezo wao wa kwanza wa tangulizi dhid ya Senegal na
michezo mingine inayofuatia.
Mbunge wa Viti Maalumu,Mheshimiwa Salma Kikwete,akizungumza
leo kwa niaba ya wabunge wengine alisema:
“Napenda kuwapongeza sana kwa kazi kubwa na nzuri kuanzia
mwanzo na hatimaye kesho tunafikia kileleni,tumekuja hapa kwa ajili ya kuungana
na timu kuwatia moyo na kuwatia shime na kuwaambia kwamba tumekuja Misri sio
kushiriki bali kushinda,”alisema na kuongeza:
“Ushirikiano katika timu yaani ‘team work’ ndiyo itakayoleta
ushindi,kwa maana hiyo Watanzania wote macho na masikio yao ni kwenu,
kwahiyo,mtangulizeni Mwenyezi Mungu na Mungu atawasaidia.”
Kwa upande wa Mheshimiwa Magreth Sitta alisema, ”Nawapongeza
sana vijana ambao wamechaguliwa katika hii timu,siku zote mi huwa napenda
kuchukua mfano wa Leicester City ya England,wakati inachukua ubingwa haikuwa na
mchezaji hata mmoja ambaye anajulikana sana,lakini waliweza kupambana kwahiyo
na nyie msigope majina naamini mnaweza.”
Wabunge hao walifunga mazungumzo yao kwa sala ya pamoja na
wa chezaji na viongozi,kwa sala iliyoongozwa Mheshimiwa Mchungaji Peter
Msigwa,kwa ajili ya kuiombea timu ya taifa katika mchezo wa kesho na michezo
mengine miwili dhid ya Kenya na Algeria.
No comments:
Post a Comment