NA FARAJA EZRA
TAASISI ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) imepokea Hundi ya shilingi milioni 20 kutoka Jumuiya ya
Patel Samaj nchini India kwa ajili ya kusaidia gharama za upasuaji kwa
watoto wenye matatizo ya moyo.
Aidha upasuaji huo utaanza rasmi June 25 mwaka huu kwa watoto kumi wenye matatizo ya moyo ili kunusuru maisha yao.
Akipokea
Hundi hiyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda, alisema fedha hizo ni maalum kwa ajili ya
kusaidia wazazi wa watoto wasio na uwezo wa kugharimikia gharama za
upasuaji wa moyo.
Makonda aliwashukuru Jumuiya ya Patel kwa kujitoa kusaidia watoto ambao
walizaaliwa wakiwa na shida ya moyo ili kunusuru maisha yao.
"Kwa
kutambua mchango wa Jumuiya ya Patel nitachangia gharama za upasuaji
kwa watoto 60 watakaofanyiwa upasuaji kutoka mwezi jully hadi Decemba
mwaka huu ambapo kila mwezi watoto kumi watafanyiwa upasuaji katika
taasisi hiyo,"alisema Makonda.
Pia
amewataka wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia shughuli za upasuaji
kwa watoto kwa sababu baadhi ya wazazi hawawezi kumudu gharama hizo.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi alisema mwaka jana
walizaaliwa jumla ya watoto milioni mbili kati yao waliofanyiwa
upasuaji ni zaidi ya watoto elfu ishirini. Hivyo idadi ya watoto
wanaozaliwa na matatizo ya moyo huongezeka kill mwaka.
Alisema
taasisi ya JKCI pia ina hadhi ya kimataifa hivyo wanahitaji vifaa vya
kutosha ili kutoa huduma bora na kwa wakati maalum kwa wahitaji.
"Tunapokea
watu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutafuta matibabu, hivyo
tunaiomba serikali itusaidie kuchangia baafhi ya vifaa vya upasuaji
lakini pia upanuzi wa eneo la kutolea huduma,"alisema Prof. Janabi.
Pia
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Patel Samaj Harish Patel alisema wameguswa
kutoa huduma za upasuaji wa moyo hasa kwa watoto bure bila gharama
yeyote.
"Tutashirikiana
bega kwa bega na taasisi ya JKCI katika utoaji huduma hiyo kwa watoto
ili kurejesha matumaini kwa wazazi na walezi wa watoto hao,"alisema
Patel.
No comments:
Post a Comment