Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kardinal Pengo, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 50 ya Halmashauri ya walei Tanzania.
Na Janeth Jovin
ASKOFU
Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycap
Kardinal Pengo amesema kuwa waamini wa kanisani katoliki wanamchango
mkubwa katika kulifanya kanisa hilo kuwa na uhai na maendeleo kwa
ujumla.
Kardinal Pengo
ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 ya Halmashauri ya walei Tanzania
yanayotarajiwa kufanyika Juni 16 mwaka huu viwanja ya Msimbazi Center
jijini Dar es Salaam.
Alisema
licha ya michango mbalimbali ikiwamo zaka inayotolewa na waamini wa
kanisa hilo pia ndio watu pekee wanaosababisha kanisa hilo kuwa na uhai
hadi leo.
"Katika
kutambua mchango huo, Juni 16 katika viwanja vya Msimbazi Center
tutaadhimisha Jubilei ya miaka 50 ya halmashauri ya Walei Tanzania watu
ambao wamekuwa wakiwaongoza vema waamini wetu katika kufanya mambo
mbalimbali yanayohusu Kanisani na jamii.
Hatua
waliopiga ya kuwafanya waamini watoe michango yao, kukaa kwa pamoja na
kuelewana tena kwa kufanya kazi kwa weledi hakika ni kubwa mno,
tunawashukuru na kumshukuru Mungu kwa hilo, " alisema.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei Taifa, Gasper Makiluli
alisema maadhimisho ya Jubilei hiyo yanawapa nguvu ya kuendelea
kufanyakazi kwa bidii na kwa kushirikiana.
Mkuu
wa Idara ya Walei Baraza la Maaskofu Tanzania Padri Raphael Madinga
alisema uwepo wa Jumuiya ndogo ndogo ni moja ya mafanikio yanayodhirisha
kazi zinazofanywa utume huo wa walei hapa nchini.
Naye
Katibu Msaidizi wa halmashauri hiyo, Donesta Byanigaba alisema
maadhimisho ya Jubilei hiyo yataanza kwa maandamano Juni 16 mwaka huu
katika Kanisa la St Joseph, Magomeni na Buguruni kuelekea Msimbazi
Center mahali ambapo ibada ya misa takatifu itakapoadhimishwa.
No comments:
Post a Comment