HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 03, 2019

SERIKALI: TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA CRDB


Sheikh Himid Jongo akiwaongoza wateja na wageni mbalimbali katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB na kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Ally Laay na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela.

Sheikh Himid Jongo akiwaongoza wageni mbalimbali katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB na kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia), akijumuika na wateja na wadau mbalimbali kupata futari.
Wageni wakipata futari.

Wageni mbalimbali wakijumuika katika futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB.

Meza Kuu.

Wanawake wakipata futari.

Wageni wakipata futari.

Wageni mbalimbali wakipata futari.

Watu mbalimbali wakipata futari.

Watoto wa kituo cha Yatima Kigamboni wakisoma utenzi.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Abdul Mohamed (kushoto), akibadilishana mawazo na mmoja wa wadau waliofika katika hafla ya futari.

Sheikh Himid Jongo akitoa hotuba yake katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akitoa hotuba yake katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wateja wake na wadau mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akipongezwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Esther Kitoka.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay, amkitoa hotuba yake katika hafla ya futari.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay, akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji kutoa hotuba yake.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, akitoa hotuba yake.

Waziri wa Mali Asili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay, akipeana mkono na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, akiomba dua.

Kuomba dua.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo wakiomba dua.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Abdul Mohamed.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.
Picha ya kumbukumbu.

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya kumbukumbu.



Na Irene Mark

SERIKALI imeahidi kuendelea kufanyakazi kwa Karibu na Benki ya CRDB huku ikitaka wadau wengine kuiunga mkono benki hiyo kwa kuwa inarudisha faida kwa jamii.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati benki hiyo ilipowafuturisha watoto yatima wa Kituo cha Safina, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijaji alisema nidhamu ya kurejesha kwa jamii ni msingi bora wa upendo kwa taifa.

"Serikali inaishukuru sana CRDB kwa kutuunga mkono kwenye miradi yetu mikubwa nasi tunaahidi hatutawaacha tutashirikiana nanyi begs kwa bega kuhakikisha mnapata mazingira bora ya kufanyia biashara.

"...Mnafanya vizuri sana kwa kurejesha faida mnayopata kwa jamii. Hili si jambo dogo tunasema endeleeni kutenda, mlipo na serikali yenu ipo endeeleeni kusimama imara zingatieni misingi ya utawala bora," alisema Naibu Waziri Kijaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema siri ya mafanikio ya benki hiyo ni umoja na ushirikiano wanaopata kutoka kwa serikali, wateja, Bodi ya Wakurugenzi na wafanyakazi wote.

Alisema ni utaratibu wa kila mwaka wa CRDB kurejesha sehemu kubwa ya faida yake kwa jamii huku akiahidi kuendelea kufanya hivyo.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Alli Laay aliiomba jamii kujitolea kuwalea watoto yatima kwa upendo kwa kuwa nao ni sehemu ya taifa hili.

No comments:

Post a Comment

Pages