HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 03, 2019

WAZIRI MKUU AUSHUKURU UONGOZI WA KANISA

*Ni baada ya kutoa sehemu ya eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa shule
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Paroko wa Parokia ya Mnacho wilayani Ruangwa, Padri Gerold Nyagau wakimsikiliza Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa wakati alipozungumza baada ya Ibada ya Jumapili kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Mnacho, Juni 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia iliyopo Mnacho wilayani Ruangwa, Juni 2, 2019. Kushoto ni Mkewe Mary na kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu  David Mwakalobo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Paroko wa Parokia ya Mnacho, Padri Gerold Nyagau (wa pili kushoto) wakati alipokagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia iliyopo Mnacho wilayani Ruangwa, Juni 2, 2019. Kushoto ni Mkewe Mary na kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu David Mwakalobo.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimina na Watawa wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mnacho baada ya Waziri Mkuu, kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia wilayani Ruangwa, Juni 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimina na Bibi Agnes Venance (kulia) na BW.  Paskazi Mashimo (katikati) ambao alisoma nao katika Shule ya Msingi ya Mnacho wilayani Rungwa kwenye miaka ya 70 .  Alisalimiana na wanafunzi wenzake hao baada ya kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia iliyopo Mnacho wilayani Ruangwa, Juni 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 

Lindi, Tanzania

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameushukuru uongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Lindi kwa kutoa sehemu ya eneo lake na baadhi ya majengo kwa ajili ya ujenzi wa shule.

Jimbo Katoliki la Lindi limetoa eneo hilo lilipo katika Parokia ya Mnacho wilayani Ruangwa ambalo awali ilikuwa shule ya msingi ya Mnacho sasa imebadilishwa na kuwa sekondari.

Waziri Mkuu ametoa shukurani hizo leo (Jumapili, Juni 2, 2019) alipokwenda kwenye kanisa Katoliki la Theresia wa Mtoto Yesu, Parokia ya Mnacho kuwasalimia waumini.

Amesema lengo la kuibadilisha shule hiyo kuwa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia ni kuwawezesha watoto wa kike wa Wilaya hiyo kusoma katika mazingira mazuri.

Waziri Mkuu ambaye ameambatana na Mkewe Mary amesema shule hiyo ya bweni itawapunguzia vishawishi watoto wa kike, hivyo kuwawezesha kutimiza malengo yao. 

Awali, uongozi wa Parokia hiyo uliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuboresha huduma za jamii zikiwemo za afya, elimu pamoja na miundombinu katika wilaya hiyo.

Naye, Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa amewaomba viongozi wa dini washikamane na wahakikishe wanatatua changamoto ya mmomonyoko wa maadili.

Amesema changamoto ya mmomonyoko wa maadiji katika jamii hususani kwa vijana ni kubwa, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha kwamba wanawarejesha kwenye maadili bora.

Kadhalika, Waziri Mkuu amekagua ujenzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia na amesema kwamba ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wake.

Shughuli zinazoendelea katika shule hiyo ni pamoja na ujenzi wa mabweni, vyumba vya madarasa, maabara na nyumba nne za walimu ambazo tayari ujenzi wake umekamilika.

No comments:

Post a Comment

Pages