HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 23, 2019

MAAFISA WA SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) WAVIKWA VYEO VYA KIJESH

Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwavisha vyeo vinavyoendana na mfumo wa Jeshi'Usu katika uendeshaji wa Shirika hilo kwa Maafisa Uhifadhi Wakuu 19 na Maafisa Uhifadhi Waandamizi 80.
Baadhi ya Maafisa Uhifadhi Wakuu na Maafisa Uhifadhi Waandamizi  wakiwa katika hafla hiyo.
Naibu Kamishna Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara,William Mwakilema akizungumza wakati wa hafla ya kuwavisha vyeo vipya Maafisa Wakuu wa Uhifadhi na Maafisa Uhifadhi Waandamizi,hafla iliyofanyika eneo la Mto wa Mbu .
Baadhi ya Maafisa Uhifadhi Wakuu .
 Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mawasiliano -TANAPA,Pascal Shelutete akitoa maelezo namna ambavyo zoezi la uvikwaji wa vyeo vipya kwa Maafisa Uhifadhi Wakuu na Maafisa Uhifadhi Waandamizi pamoja na Kiapo cha Utii .
 Maafisa Uhifadhi Wakuu na Maafisa Uhifadhi Waandamizi wa Jeshi'Usu la Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakila kiapo wakati wa hafla fupi ya kuwavisha vyeo vipya vya nafasi hizo ,hafla iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mto wa Mbu -Karatu mkoani Manyara.
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt, Allan Kijazi akiwavisha vyeo Maafisa Uhifadhi Wakuu wa Jeshi Usu -TANAPA,wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika shule ya Msingi Mto wa Mbu  wilayani Monduli .Maafisa Uhifadhi Wakuu 19 walivishwa vyeo vipya.
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt, Allan Kijazi akiwavisha vyeo Maafisa Uhifadhi Waandamizi wa Jeshi'Usu -TANAPA,wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika shule ya Msingi Mto wa Mbu  wilayani Monduli .Maafisa Uhifadhi Waandamizi  80 walivishwa vyeo vipya .
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt ,Allan Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  Maafisa Uhifadhi Wakuu wa Jeshi Usu -TANAPA,mara baada ya kula kiapo na kuvishwa vyeo vipya .Maafisa Uhifadhi Wakuu 19 walivishwa vyeo vipya . 
Kamishna Mkuu wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  Maafisa Uhifadhi Waandamizi wa Jeshi Usu -TANAPA,mara baada ya kula kiapo na kuvishwa vyeo vipya .Maafisa Uhifadhi Waaandamizi 80 walivishwa vyeo vipya .

Na Dixon Busagaga

KAMISHNA wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) (CC) Dkt,Allan Kijazi amewavisha vyeo vipya Maafisa Uhifadhi Wakuu na Maafisa Uhifadhi Waandamizi,vyeo vinavyoendana na mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa shirika hilo kutoka ule wa kiraia na kuwa Jeshi Usu.

Zoezi la uvishwaji vyeo kwa Maafisa hao 99 wa vitengo mbalimbali katika shirika hilo limefanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Mto wa Mbu,wilayani Karatu na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa kamati za ulinzi na usalama za wilaya.

Akizungumza mara baada ya Maafisa hao kula kiapo cha Utii ,Kamishna wa Uhifadhi –TANAPA ,(CC) Dkt Kijazi aliwataka kuhakikisha suala la ulinzi na usalama wa Hifadhi unaimarika zaidi pamoja na kushirikiana na wananchi katika kulinda rasilimali za taifa .

“Ni wakati wa kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya ujangili na hii ni kutokana na kasi ya matukio ya ujangili kuongezeka katika baadhi ya hifadhi”alisema Dkt Kijazi .

Vyeo vipya vimetolewa wa Maafisa Uhifadhi Wakuu 19 na Maafisa Waandamizi 80 ikiwa chachu ya kuendelea na majukumu yao wakiwa katika mfumo wa utendaji kazi wa Jeshi Usu.

No comments:

Post a Comment

Pages