HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 03, 2019

MKE, MUME WAHUKUMIWA

Na Janeth Jovin

MKURUGENZI wa kampuni ya Biabana,  Anna Kristina Edler, (54) na mume wake, Anders Svensson 58   wamehukumiwa kulipa faini ya sh. Milioni 20 au kwenda jela  mwaka mmoja na nusu baada ya kukiri tuhuma za kuajiri raia wa nje ya nchi na kujihusisha na kazi bila ya kuwa na kibali nchini

Hukumu hiyo imesomwa, leo Juni 3,2019 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo washtakiwa hao raia wa Swideni wanakabiliwa na mashtaka mawili, likiwemo la kufanya kazi nchini bila ya kuwa na  kibali.

Hata hivyo, baada ya kusomewa mashtaka  yao, washtakiwa wamekili na wamehukumiwa kulipa faini ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na nusu gerezani.

 Mapema akisoma mashtaka yao, wakili wa serikali, Daisy Makakala amedai kati ya Agosti 18 mwaka Jana na Aprili 3, 2019 huko Mikocheni, mshtakiwa Elder,  akiwa kama mkurugenzi wa kampuni ya Biabana Ltd alimuajiri Anders na kufanya kazi  katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali kutoka idara yavUhamiaji.

Katika shtaka la pili imedaiwa, aiku na mahali hapo mshtakiwa Enders alijihusisha na kazi kama muajiriwa wa kampuni ya Biabana LTD bila ya kuwa na kibali kinachotolewa na idaravya Uhamiaji.

No comments:

Post a Comment

Pages