Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y.
Maselle (kushoto), Mhandisi Jairos Nkoroka (wa tatu kulia) pamoja na
wafanyakazi wakikagua propella za vivuko vilivyohifadhiwa katika
karakana ya mji wa Ifakara baada ya daraja la mto Kilombero
kukamililika. Vivuko hivyo, MV. Kilombero I na II vitaanza kukarabatiwa
na kuunganishwa hivi karibuni tayari kwa hatua ya kupelekwa katika eneo
la Kikove Malinyi kwa ajili ya kutoa huduma.
Mhandisi
Jairos Nkoroka kushoto akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle mashine ya kugandamiza
vipuri vya magari (press machine) wakati alipotembelea kukagua utendaji
kazi wa karakana hiyo mpya ya TEMESA iliyoanza kutoa huduma mwezi Juni
mwaka huu katika Halmashauri ya mji wa Ifakara wilayani Kilombero mkoani
Morogoro. Karakana hiyo sasa itahudumia wilaya zote za karibu ikiwemo
wilaya ya Ulanga na Malinyi ambazo awali zilikuwa zikitegemea kupata
huduma Morogoro mjini.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle
(kulia), akikagua mashine ya kupimia uwiano wa matairi ya magari (wheel
balance) iliyopo katika karakana ya TEMESA katika Halmashauri ya mji wa
Ifakara wakati alipoitembelea kujionea utendaji kazi wake mara baada ya
kuanza kutoa huduma Juni mosi mwaka huu. Karakana hiyo sasa itahudumia
wilaya zote za karibu ikiwemo wilaya ya Ulanga na Malinyi ambazo awali
zilikuwa zikitegemea kupata huduma za matengenezo ya magari na mitambo
kutoka Morogoro mjini.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle
(wa pili kushoto) akifurahia jambo na wafanyakazi mara baada ya kumaliza
kukagua mipaka ya karakana ya TEMESA Ifakara iliyoanza kutoa huduma
Juni mosi mwaka huu katika Halmashauri ya mji wa Ifakara wilayani
Kilombero mkoani Morogoro. Karakana hiyo sasa itahudumia wilaya zote za
karibu ikiwemo wilaya ya Ulanga na Malinyi ambazo awali zilikuwa
zikitegemea kupata huduma za matengenezo ya magari na mitambo kutoka
Morogoro mjini.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle
(kulia), akikagua kivuko cha MV. Kilombero I kilichohifadhiwa katika
karakana ya mji wa Ifakara baada ya daraja la mto Kilombero
kukamililika. Kivuko hicho pamoja na kivuko cha MV. Kilombero II
vitaanza kukarabatiwa na kuunganishwa hivi karibuni tayari kwa hatua ya
kupelekwa katika eneo la Kikove Malinyi kwa ajili ya kutoa huduma.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle
kushoto akikagua kivuko cha MV Kilombero II ambacho kimehifadhiwa katika
karakana hiyo baada ya huduma za kivuko kufungwa katika mto Kilombero
kutokana na kukamilika kwa daraja. Kivuko hicho pamoja na kivuko cha MV.
Kilombero I vinatarajiwa kuanza kufanyiwa ukarabati tayari kwa hatua ya
kupelekwa katika eneo la Kikove Malinyi kwa ajili ya kutoa huduma
katika maeneo hayo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y.
Maselle katikati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa karakana
mpya ya TEMESA iliyopo katika Halmashauri ya mji wa Ifakara wilayani
Kilombero mara baada ya kumaliza kukagua karakana hiyo. (Picha na Alfred Mgweo- TEMESA).
No comments:
Post a Comment