Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii .Constantine Kanyasu kushoto akimsikiliza kwa umakini Meneja wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
wakati alipotembelea alipokwenda kufunga maonyesho ya saba ya
biashara ya kimataifa yaliyokuwa yakiendelea kwenye viwanja vya
Mwahako Jijini Tanga.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii .Constantine Kanyasu kushoto akimsikiliza kwa umakini Meneja wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu wakati
alipotembelea alipokwenda kufunga maonyesho ya saba ya biashara ya
kimataifa yaliyokuwa yakiendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii .Constantine Kanyasu kulia akipima uzito kwenye banda la Mfuko
wa Taifa wa Bima Afya mkoani Tanga (NHIF) mara baada ya
kulitembelea.
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF)
Ally Mwakababu kushoto akitoa elimu juu ya CHF iliyoboreshwa mkazi wa
Tabata Jijini Dar es Salaam ambaye alitembelea banda lao Devutia
Kulembeka.
Mhudumu wa Afya kulia akiendelea na shughuli kwenye banda hilo.
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakipima afya zao.
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakipima afya zao.
Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga
umetumia maonyesho ya saba ya biashara ya kimataifa kutoa elimu kwa
wananchi kuhusiana na CHF iliyoboreshwa ili waweze kujiunga nayo na
kuweza kunufaika.
Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko huo
mkoani hapa Ally Mwakababu wakati akizungumza na waandishi wa habari
kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.
Alisema wameona
washiriki kwenye maonyesho hayo ili pia kutoa elimu ya bima ya afya
kwa watumishi, wananchi binafasi, wanafunzi na watoto ikiwa ni mkakati
wao wa kufikia watu wengi zaidi
“Tunashukuru kwenye
maonyesho haya tumepata fursa ya kutoa elimu ya CHF iliyoboreshwa na
nia kubwa ni kwamba kila mwananchi awe na kinga ya matibabu wakati
wote”Alisema
Meneja huyo alisema licha ya kutoa elimu hiyo
lakini pia wanafanya zoezi la kupima afya za wananchi wanaotembelea
banda lao ikiwemo kupima uzito lakini pia wanapima sukari na baadae
kutoa ushauri wa wananchi wanaopita kwenye banda lao.
Alieleza ushauri huo ni kwamba baada ya kupimwa wanatakiwa kufanye
nini hivyo wanaamini wananchi wakitumia banda hilo watapata huduma ya
vipimo bure na kupata ushauri mzuri.
No comments:
Post a Comment