Mtaalamu Mwandamizi wa Vipaji, Mafunzo na uendelezaji wa benki ya NMB, Edith Mwiyombela, kizungumza wakati wa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri Tanzanja (ATE), Taasisi ya CEFA na CCBRT kwa wahitimu wenye ulemavu waliyoifanya Makao makuu ya benki hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu, Emmanuel Akonaay akifafanua jambo wakati wa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa kushirikiana na Chama Cha Waajiri Tanzanja (ATE), Taasisi ya CEFA na CCBRT kwa wahitimu wenye ulemavu iliyofanyika mwishoni mwa wiki Makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkuu wa Kitengo Cha Taaluma ndani ya Rasilimali Watu, Joanitha Rwegasira Mrengo akieleza jambo kwenye ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa kushirikiana na Chama Cha Waajiri Tanzanja (ATE), Taasisi ya CEFA na CCBRT kwa wahitimu wenye ulemavu waliyoifanya jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu Mwanadamizi Uajiri wa Benki ya NMB, Eleanor Maseke akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa kushirikiana na Chama Cha Waajiri Tanzanja (ATE), Taasisi ya CEFA na CCBRT kwa wahitimu wenye ulemavu waliyoifanya katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja.
Mwakilishi
kutoka Taasisi ya CEFA, Mratibu Mkuu wa Uwezeshaji Kiuchumi, Gerald
Mpangala ametoa wito kwa Taasisi mbalimbali kutoa mafunzo kama hayo kwa
kuwapa Watu hao wenye Ulemavu mafunzo mbalimbali ikiwemo ya Kiuchumi,
amewataka Wanafunzi watano waliopata nafasi hiyo kwenye Benki ya NMB
kutumia ipasavyo nafasi hiyo kufunza.
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Benki
ya NMB imetoa nafasi tano kwa watu wanaoishi na ulemavu kujifunza
masuala tofauti ndani ya benki hiyo katika Idara zake mbalimbali kwa
kipindi cha awali cha miezi mitatu.
Benki
hiyo imetoa nafasi hizo wakati wa uzinduzi wa mpango maalum ujulikanao
kama 'All Inclusive' kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri Tanzania
(ATE) na Taasisi ya CEFA inayojihusisha na watu wenye Ulemavu pamoja na
Hospitali ya CCBRT ya Dar es Salaam.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha
Rasilimaliwatu kutoka Benki hiyo, Emmanuel Akonaay amesema wametoa
nafasi hizo kwa kuangalia ujuzi,mafunzo na elimu zao ambapo watapata
nafasi ya kupata mafunzo kwa vitendo katika idara tofauti za benki hiyo.
Akonaay
amesema NMB inaamini uwezo wa mtu uko kwenye kipaji na sio muonekano
wake wa nje, amesema wametoa nafasi hizo kwa kwa watu wa jamii hiyo
kuonyesha vipaji na baadae kutoa ajira kwao pale kutakapokuwa na
uhitaji.
Kwa
Upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Taaluma ndani ya Rasilimali watu
kutoka Benki ya NMB, Joanitha Rwegasira amesema wamepokea Watu 25
watakaopata mafunzo hayo katika masuala ya Kifedha na masuala mbalimbali
yakibenki.
Naye
Mmoja wa Watu wanaopata mafunzo hayo, Mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa
Jamii, Faudhia Kitenge amesema amepata nafasi yakujifunza masuala
mbalimbali ya utendaji wa kibenki.
Faudhia
ametoa wito kwa Taasisi nyingine kutoa nafasi kama hizo kwa Watu wenye
Ulemavu ili kutoa nafasi kwa kundi hilo kuonyesha vipaji na uwezo kwa
jamii.
No comments:
Post a Comment