Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa (Mb)
akikagua baadhi ya nyumba za
makazi zilizojengwa Bunju B mkoani Dar es Salaam kwa ajili ya
kuuza na kuwapangisha Watumishi wa Umma na Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi za
Jamii.
Dar es Salaam, Tanzania
Serikali imeendelea
kuwajali Watumishi wa Umma nchini kwa kuwajengea nyumba bora za gharama nafuu
kupitia miradi ya ujenzi wa nyumba inayotekelezwa na Watumishi Housing Company
katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwawezesha watumishi kumiliki nyumba bora
za kuishi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa (Mb) alipotembelea miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi Gezaulole Kigamboni na Bunju B mkoani Dar es Salaam.Mhe. Dk. Mwanjelwa amesema, amejionea nyumba zilizojengwa kisasa, gharama nafuu na zenye viwango vinavyostahili kwa makazi ya watumishi wa umma na wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii ambao ndio walengwa wakuu wa miradi hiyo.
Aidha, Mhe. Dk. Mwanjelwa amewaagiza watendaji wa Watumishi Housing Company kuhakikisha wanakuwa na mkakati madhubuti wa kutoa taarifa kwa watumishi wa umma juu ya uwepo wa nyumba zilizojengwa na kampuni hiyo, sehemu zilipo na bei elekezi kwa wanaohitaji kununua, ikiwa ni pamoja na bei ya kupangisha.
Mhe. Dk.
Mwanjelwa amekamilisha ziara yake ya kikazi mkoani Dar es Salaam ya kukagua
miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Watumishi wa Umma na wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na
kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji wa Watumishi Housing Company.Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa (Mb) alipotembelea miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi Gezaulole Kigamboni na Bunju B mkoani Dar es Salaam.Mhe. Dk. Mwanjelwa amesema, amejionea nyumba zilizojengwa kisasa, gharama nafuu na zenye viwango vinavyostahili kwa makazi ya watumishi wa umma na wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii ambao ndio walengwa wakuu wa miradi hiyo.
Aidha, Mhe. Dk. Mwanjelwa amewaagiza watendaji wa Watumishi Housing Company kuhakikisha wanakuwa na mkakati madhubuti wa kutoa taarifa kwa watumishi wa umma juu ya uwepo wa nyumba zilizojengwa na kampuni hiyo, sehemu zilipo na bei elekezi kwa wanaohitaji kununua, ikiwa ni pamoja na bei ya kupangisha.
IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 02 JUNI, 2019
No comments:
Post a Comment