Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
TFDA, Adam Fimbo.
Na Asha Mwakyonde
MAMLAKA
ya Dawa na Chakula Tanzania (TFDA), imesema kuwa imeweka mfumo thabiti
wa udhibiti kwa lengo la kuhakikisha chakula kinachozalishwa ndani ya
nchi na kile kinachoingizwa kinakidhi vigezo vya usalama na ubora ili
walaji wasipate madhara kiafya.
Pia wanahabari wametakiwa kuwa mabalozi wa kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa masuala ya usalama wa Chakula.
Haya
yalisemwa Wilayani Bagamoyo Pwani na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
TFDA, Adam Fimbo wakati wa ufunguzi wa semina ya kuelimisha wanahabari
kuhusu masuala ya usalama wa chakula.
Mkurugenzi
huyo alisema kuwa madhara mengi yatokanayo na chakula kisicho salama
huchangiwa kwa kiasi kikubwa na uelewa mdogo wa jamii juu ya masuala ya
usalama wa chakula na kutozingatia ipasavyo kanunu za upatikanaji
chakula salama.
Alitolea
mfano baadhi vinasababishwa na uelewa mdogo miongoni mwa jamii
kuwa ni uandaaji wa chakula katika mazingira yasiyo safi, kutonawa
mikono kwa maji safi na sabuni baada ya kutoka chooni, kabla ya kuandaa
chakula.
"Kwa mantiki hii
elimu kwa umma juu ya kuhakikisha usalama wa chakula katika hatua
mbalimbali za mnyororo wa chakula ni muhimu katika kuleta mabadiliko
chanya," alisema Fimbo.
Aliongeza
kuwa kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), takimwimu zinaonesha
takribani watu milioni 600 sawa na mtu mmoja kati ya 10 huugua kila
mwaka kutokana na kula Chakula kisicho salama.
Mkurugenzi
Fimbo alifafanua kuwa kati yao 420,000 hufariki na kwamba kati ya hao
watoto ni 125,000 wenye umri chini ya miaka mitano.
Kwa
upande wake Mkaguzi Mkuu wa chakula kutoka mamlaka hiyo, Lazaro
Mwambole alisema kuwa tayari TFDA ilishawafikia wajasiriamali 1500 kwa
kutoa elimu juu ya masuala ya usalama wa Chakula katika mikoa mitano.
Alisema
mwaandaji wa chakula kabla hajaanza kuandaa anatakiwa kupimwa Afya na
kwamba wenngi wao wanaogopa kupima wakidhani wanapimwa ukimwi ndio maana
huogopa.
"Changamoto
kubwa iliyopo kwa waandaaji wa chakula baadhi yao wanatabia ya kuongea
sana, kujikuna wakati kuundaa Chakula,"alisema.
No comments:
Post a Comment