Baadhi ya wajane wakiwa katika maandamano ya
kusheherekea Siku ya wajane Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wajane na wagane
katika maadhimisho ya Siku ya Wajane yalioyofanyika jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Naibu Waziri wa Afyaya, Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile ametoa rai kwa Wizara yake na TAMISEMI kutoa elimu kwa Jamii
hususani kuhusu mirathi na uandishi wa wosia ili jamii iweze kutambua umuhimu wa mirathi na
wosia na kuondokana na migogoro mingi inayowakumba wajane Nchini.
Naibu Waziri Ndugulile ameyasema hayo leo wakati wa
Maadhimisho ya Siku ya Wajane Duniani yaliyofanyika Kitaifa leo Jijini Dodoma
na kusisitiza kuwa elimu ya mirathi na uandishi wa wosia ni muhimu kwa sababu
idadi kubwa ya watu bado haijui haki zake.
Aidha Dkt. Ndugulile amewataka wanandoa kote Nchini kuhakikisha
wanasajili ndoa zao ili wajane na watoto waweze kupata haki zao lakini pia
akawataka wananchi kuiga mfano wa Nchi za Ulaya ambapo kabla ya kufunga ndoa
kila mmoja utaja mali zake ili zisiwe sehemu ya mirathi inapotokea kuna
kufarakana au mmoja kufariki.
Dkt. Ndugulile ameonya kuwa maandalizi ya mirathi na wosia
yaanze sasa bila kusubiri vifo na kuwataka watu kufahamu kuwa mtu kuwa mjane
sio mwisho wa maisha bali watambue kuwa mwenzako anapoondoka maisha yanapaswa
kusonga mbele.
Aidha Naibu Waziri Ndugulile amewataka wadau wote Nchini
kukutana na Wizara yake ili kupitia Sera ya Taifa ya maendeleo ya Wanawake na Jinsia
na kuahakikisha masuala yote ya mirathi
na ukatili wa kijinsia yanazingatiwa kulingana na wakati huo akiwataka
wasanii kutumia sanaa yao kuelimisha umma kuhusu madhira na madhara yawakutayo
wajane hao.
Aidha Mgane wa Kiume Bw. Eliona Makundi akitoa ushuhuda wake
kwa wanaume wafiwa ameonya wanaume
kutokimbilia kuoa bali watunze watoto wao mpaka wafikie ndoto zao kwani ukikosa
umakini mwanamke wa kambo anaweza akasababisha familia kusambaratika.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt.
John Jingu amesema kuwa maadhimisho haya yanafanyika Jijini Dodoma kwa mara ya
kwanza Kitaifa na yamewakutanisha Wajane wote kutoka mikoa 20 ya Tanzania bara
na Wizara yake imewapatia fursa ya kuwajengea uwezo wajane hao kuhusu
ujasiliamali na stadi mbalimbali za maisha.
Katibu Mkuu Jingu ameongeza kuwa azimio la kuitambua tarehe
23 Juni kuwa Siku ya Wajane Duniani ni kutokana na Changamoto mbalimbali
ikiwemo umasikini, unyanyapaa na kudhulumiwa haki zao za msingi za kijamii na
kiuchumi na kuongeza kuwa dunia kwa sasa ina zaidi ya wajane 258 milioni na
mmoja kati ya Wajane 10 wanaishi katika umasikini wa kutupwa.
Maadhimisho haya yanafanyika Duniani kote kwa lengo la kutoa
Msukomo kwa Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za makusudi
kutokomeza umasikini na uonevu unaowakabili wajane kote Duniani.
No comments:
Post a Comment