
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akizungumza na watumishi wa ofisi yake wanaotarajia kustaafu hivi karibuni wakati wa mafunzo ya maandalizi ya kustaafu yaliyoendeshwa na wakufunzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma.Mafunzo hayo yalifanyika Juni 21, 2019 Jijini Dodoma.

Mkufunzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Bi. Ziada Sadick akizungumza jambo kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu hivi karibuni wakati wa mafunzo ya ya maandalizi ya kustaafu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma inayoendelea.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akimkabidhi cheti cha mafunzo ya maandalizi ya kustaafu Mtunza Kumbukumbu Mkuu wa ofisi hiyo Bi. Amina Simbaulanga ambaye anatarajia kustaafu mwezi mwishoni mwa mwaka huu.
Na
Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Waziri Mkuu na Bunge) Bi.Maimuna Tarishi amewaasa watumishi wa Ofisi hiyo
wanaotarajia kustaafu hivi karibuni kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa
weledi hadi siku zao za kuhitimisha utumishi wao katika Ofisi hiyo zitakapofika.
Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha
mafunzo ya kujiandaa kustaafu yaliyoandaliwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
wiki ya utumishi wa umma yanayoendelea aliwaeleza umuhimu wa kuendelea
kuwajibika kulingana na taratibu na kanuni zinazoongoza utendaji kazi wa kika
siku.
“ Hatutarajii kuona kati yenu
hata mmoja wenu akianza kuchelewa kazini au kuanza kuzembea katika
kutekeleza majukumu yake kwa kuwa
anatarajia kustaafu mwaka huu, tunatarajia kuwa sasa mtaendelea kuongeza kasi
ya kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuwarithisha utamaduni wa kupenda
kufanya kazi kwa bidii wale wanaobaki” Alisisitiza Bi Maimuna.
Akifafanua amesema kila mtumishi
wa umma anayetarajia kustaafu anapaswa kuhakikisha kuwa anaendelea kuonesha mfano
bora katika sehemu yake ya kazi kwa kutekeleza yale anayotakiwa kwa weledi na
kwa wakati akizingatia maslahi ya nchi.
Aliwaasa watumishi hao kutumia
vizuri elimu waliyopatiwa kupitia mafunzo yakuwaandaa kustaafu yaliyoandaliwa
na Ofisi hiyo ili hatimaye wanapostaafu waweze kuanzisha na kuendeleza shughuli
za uzalishaji katika maeneo yao.
Kwa upande wake Mkufunzi kutoka
chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni Bi. Ziada Sadick amesema kuwa Chuo hicho
kinaipongeza Ofisi yan Waziri mkuu kwa kuandaa mafunzo hayo kwa watumishi wake
wanaotarajia kustaafu hivi karibuni.
Aliongeza kuwa mafunzo haya
yanawapa uwezo watumishi hao katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza
zikawakabili baada ya kustaafu.
Katika mafunzo hayo watumishi
wanaotarajia kustaafu waliweza kujifunza
masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuanzisha miradi ya uzalishaji, mbinu za
kukabilina na msongo wa mawazo na mada nyingine mbalimbali.Mafunzo hayo
yalishirikisha watumishi takribani ishirini wa kada mbalimbali.
No comments:
Post a Comment