Mstahiki Meya wa Jiji la
Dodoma, Prof Davis Mwamfupe, akieleza umuhimu wa kuzingatia mbinu za ufanyaji
wa tafiti zenye kuzingatia viwango vya kimataifa katika ,wakati akifungua
warsha ya watafiti kutoka nchi tano za Afrika, katika Chuo cha Mipango ya
Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda, akitoa mada katika warsha ya watafiti kutoka nchi tano
za Afrika, katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma,
ambapo alieleza mikakati ya Serikali kukuza uchumi na ajira nchini.
Watafiti kutoka nchi ya
Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Rwanda na wenyeji Tanzania, wakifuatilia mada
kuhusu changamoto za kiuchumi Afrika na mikakati ya kukabiliana nayo ikiwemo
kuwa na uchumi wa viwanda, iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na
Utalii Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani), katika
Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
Na Peter Haule na Farida Ramadhani WFM, Dodoma
Watafiti nchini wametakiwa
kuweka mkazo katika mbinu za utafiti zinazokidhi viwango vya kimataifa ili kuwa
na majibu ya tafiti zenye tija zilizo na lengo la kutatua changamoto katika
jamii ya watanzania na duniani kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa na Mstahiki
Meya wa Jiji la Dodoma, Prof Davis Mwamfupe, alipokuwa akifungua warsha ya Watafiti
kutoka nchi ya Kenya, Afrika Kusini, Rwanda, Uganda na wenyeji Tanzania,
uliofanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
Mtahiki Meya Mwamfupe,
alisema kuwa ili utafiti uwe na thamani nilazima kutumia mbinu zinazoaminika
bila kujali utafiti unaofanyika unahusu kitu gani, kwa lengo la kuondoa
mkanganyiko wa matokeo hivyo kuwa na tija kwa jamii.
“Utafiti wa kisayansi ni
ule unaotumia njia zinazokubalika kimataifa na kuwa na uwezo wa kukabiliana na
changamoto zikiwemo za kutokuwa na usawa hasa katika pande mbili za Dunia yani
Kasikazini na Kusini lakini pia katika jamii moja na nyingine”, alieleza Meya
Prof. Mwamfupe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda, ambaye alikua mtoa mada katika warsha hiyo alisema
kuwa, katika wasilisho lake wadau kutoka nje ya nchi wamefurahishwa na
uchambuzi kuhusu hali ya uchumi ambapo ilielezwa namna watu wenye kipato
kikubwa kupenda kununua bidhaa nje jambo ambalo limeifanya Serikali ya Tanzania
kuweka mikakati ya kutatua tatizo hilo ili kujenga uchumi wa bnchi.
Alisema kuwa tabia ya
wenye kipato kikubwa kununua bidhaa nje kuna kosesha ajira, hivyo Serikali
imeamua kuweka mikakati ya Ujenzi wa uchumi katika Nyanja ya viwanda, kilimo na
miundombinu ikiwemo ya umeme, jambo ambalo ni ajenda ya Afrika
Kwa upande wake Mratibu wa
Warsha hiyo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Cha Mipango Vijijini, Dkt. George
Kanyasi, alisema kuwa lengo la Warsha hiyo ni kuwakutanisha watafiti
wanaochipukia na wanasayansi kutoka nchi tano za Afrika kwa lengo la kuwajengea
uwezo ili kupata watafiti mahiri.
Amesema kuwa kazi ya
tafiti sio tu kuongeza maarifa lakini pia kutatua changamoto katika maeneo
yaliyokosa usawa katika elimu, uchumi, siasa na masuala ya kijamii
Mkutano huo pamoja na
kuwashirikisha watafiti kutoka nje ya nchi, pia umewahusisha baadhi ya wadau
kutoka Halmashauri ili kujua changamoto zao na kuweka mikakati ya kuzitatua,
aidha warsha zinazofuata zitawakutanisha Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa
Mipango ili waweze kubaini matatizo ya maeneo yao na waweze kuyatatua.
No comments:
Post a Comment