Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kombe
nahodha wa timu ya soka ya Bunge, Cosato Chumi baada ya timu yake
kuibuka na ushindi wa 5-3 dhidi ya timu ya NMB katika Bonanza la Benki
ya NMB na Wabunge lililofanyika
kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimkabidhi kombe
nahodha wa timu ya Mpira wa Kikapu ya Benki ya NMB – Danford Kisinda ,
baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa vikapu 54-52 dhidi ya timu ya
mpira wa Kikapu
ya Bunge katika mechi ya Bonanza la Benki ya NMB na Wabunge
lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania – Tulia Ackson na Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB wakiwa
pamoja na timu ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakifurahia
ushindi wa timu za
bunge kwenye Bonanza la michezo la NMB na Bunge lililofanyika kwenye
uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB akishangilia
ushindi wa Mpira wa Kikapu baada ya kuwashinda timu ya Bunge kwa Vikapu
54 kwa 52 kwenye Bonanza la michezo la NMB na Bunge lililofanyika kwenye
uwanja wa Jamhuri
jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesifu juhudi za Benki ya NMB kwenye kuunganisha jamii kupitia huduma bora za kibenki,
matukio ya michezo na hata misaada mbalimbali nia ikiwa kuona jamii ya kitanzania inashiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa Taifa.
Alitoa kauli hiyo juzi jijini Dodoma kwenye Bonanza la michezo lililowashirikisha wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na wafanyakazi wa Benki ya NMB.
Akizungumzia kuhusu utendaji wa benki ya NMB, amesema imekuwa ikishirikiana na Serikali kuwaelimisha wakulima umuhimu
wa kufungua akaunti na kujiwekea akiba.
“Benki ya NMB ni benki pekee iliyomudu kufungua matawi hadi maeneo ya vijijini, hivyo kurahisishha
upatikanaji wa huduma kwa watumishi na wananchi waishio maeneo hayo.”
Amesema ni muhimu kwa watumishi kushiriki katika michezo mbalimbali kwa kuwa inaimarisha afya pamoja na kudumisha
mshikamano.
Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ni mpira wa miguu ambapo timu ya Bunge ilishinda baada ya kuifunga timu ya
benki ya NMB magoli matano kwa matatu.
Kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete timu ya Bunge iliibuka na ushindi baada ya kuifunga timu ya NMB magoli 25 kwa
18, huku katika mchezo wa mpira wa kikapu timu ya NMB ilishinda baada ya kuifunga Bunge vikapu 54 kwa 52.
Katika mchezo wa kuvuta kamba timu ya Wabunge Wanawake na Wanaume waliibuka na ushindi baada ya kuzishinda timu za
NMB.
No comments:
Post a Comment