Mtaalam Mussa Otieno, Akitoa Elimu juu ya Mfumo wa iMES, kwa wataalam wa Jiji la Mwanza.
Wataalam wa Jiji la Mwanza wakiwa wanafatili kwa makini maelezo
yaliyokuwa yakitolewa na Matoa mada juu ya Matumizi ya Mfumo wa iMES
katika Ukumbi wa Jiji la Mwanza.
Mtaalam Ismail Chami akionekana kwa mbali amesimama akitoa maelezo juu
ya ubora wa mfumo wa iMES utakavyokuwa suluhisho la taarifa huku wajumbe
wakiwa wanafatilia kwa makini.
Na Atley Kuni- Mwanza
Mfumo jumuishi wa ufatiliaji
na tathmini (intergration Monitoring and Evaluation System-iMES),
umepokelewa vizuri na wataalam wa Jiji
la Mwanza na kuuona kuwa mfumbuzi wa tatizo la taarifa na takwimu.
Wakizungumza katika
kikao cha pamoja cha kuupitia mfumo huo kwa hatua za awali kwa maeneo ya majaribio
kwenye kikao kilichofanyika ukumbi wa
jiji la Mwanza, Mtakwimu Costantine Ruhinda na Afisa mazingira Fanueli Kasenene
wote wa Jiji la Mwanza walisema, wanaiona iMES kama suluhu ya kudumu kutokana
na historia isiyoridhisha ya masuala ya takwimu na taarifa katika kipindi cha nyuma
kabla ya mfumo huu wa sasa.
Ruhinda alisema,
wamekuwa na tatizo la kitakwimu kwa kupewa takwimu zinazo tofautiana ndani ya
idara au sekta moja,
“Unaweza kupeleka
dodoso asubuhi, ukirudi jioni kulifatilia ukapewa taarifa husika, halafu nadni
ya muda mfupi siku inayofuata ukapeleke dodoso lingune, chakushangaza utakuta
chanzo hicho hicho kimoja kimekupatia takwimu mbili tofauti ndani ya muda mfupi
tu” alisema Ruhinda.
Kwa upande wake Afisa
Mazingira wa Jiji hilo, Fanueli Kasenene anaiona
iMES kama suluhu ya tatizo lakunyang’anyana rasilimali hususan ni wakati wa
upangaji wa vipaumbele vya bajeti.
“Sisi kama idara ya Usafi
na Mazingra kipaumbele kikubwa kilikuwa kinaelekezwa kwenye Idara ya Afya
wakati wa bajeti na hii ilitokana na idara hii ya Usafi wa Mazingira kuwa mpya
na viashiria vya ukiutendaji vilikuwa vipo chini ya Idara ya Afya, hivyo basi kutotoa
fursa yakutengeneza Mipango ikizingatiwa kuwa ni idara inayojitegemea”
Alisema Kasenene.
Kasenene anasema, mifano
halisi ilikuwa katika viashiria vya uzalishaji wa taka ngumu, viashiria vya
uondoshaji na usafirishaji wa taka ngumu lakini pia viashiria vya maeneo ya
wazi, maeneo yanayohifadhiwa (Environmental Protected Areas), kutooneka
ndani ya Mifumo iliyopita.
iMES ni Mfumo ulibuniwa
na kusanifiwa na Serikali kwakushirikiana na Wadau wa Maendeleo USAID chini ya
Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS.3, kwakutumia wataalam wa
ndani ya nchi.
No comments:
Post a Comment