Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua banda la maonesho la Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kwa ajili ya kujionea maandalizi ya Maadhimisho 26 ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (Nane Nane) tarehe 29 Julai 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua banda la maonesho la Mkoa Shinyanga mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kwa ajili ya kujionea maandalizi ya Maadhimisho 26 ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (Nane Nane) tarehe 29 Julai 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua zoezi la ufugaji samaki kwenye banda la maonesho la Jeshi la kujenga Taifa JKT mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kwa ajili ya kujionea maandalizi ya Maadhimisho 26 ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (Nane Nane) tarehe 29 Julai 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mazao mbalimbali katika banda la maonesho la Jeshi la kujenga Taifa JKT mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kwa ajili ya kujionea maandalizi ya Maadhimisho 26 ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (Nane Nane) tarehe 29 Julai 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mashine za kisasa za kilimo kwenye banda la maonesho la Jeshi la kujenga Taifa JKT mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kwa ajili ya kujionea maandalizi ya Maadhimisho 26 ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (Nane Nane) tarehe 29 Julai 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Simiyu
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga tarehe 29 Julai 2019 amewasili Mkoani Simiyu kwa ajili ya kujionea
maandalizi ya Maadhimisho 26 ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (Nane Nane)
yenye lengo la kuwatambua na kuwaenzi Wadau Wakuu wa Sekta ya Kilimo ambao ni
Wakulima, Wafugaji, Wavuvi, Wanaushirika, Wasindikaji wa mazao ya kilimo,
mifugo, uvuvi na maliasili kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa katika kuendeleza
uchumi wa nchi yetu.
Mwaka huu wa 2019, sherehe
hizi zinafanyika Kitaifa mjini Bariadi katika Viwanja vya maonesho ya kilimo
Nyakabindi katika Mkoa wa Simiyu hivyo Mhe Hasunga amepongeza Uongozi wa mikoa
ya Simiyu, Shinyanga na Mara kwa juhudi zao za kufanikisha kuingiza uwanjani
huduma za msingi ambazo ni maji na umeme.
Alisema kuwa jukumu hilo
kwa Serikali na Wadau wa Sekta Binafsi ni kuendeleza viwanja hivyo vya
Nyakabindi kwa kujenga mabanda ya maonesho ya kudumu na kuboresha huduma muhimu
za kijamii ili kuwe na maonesho endelevu yenye sura ya Kitaifa na Kimataifa.
Alisema kuwa Serikali kwa
kushirikiana na Wadau mbalimbali, imeendelea kuongeza na kuboresha viwanja vya
maonesho katika Kanda mbalimbali hapa nchini, kwa sasa kuna viwanja nane (8)
vya maonesho ya kilimo ambavyo ni Themi (Arusha) Kanda ya Kaskazini
inayohusisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara; Mwl. J.K.Nyerere
(Morogoro) Kanda ya Mashariki ambayo mikoa yake ni Dar es Salaam, Pwani,
Morogoro na Tanga;na John Mwakangale (Mbeya) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Ruvuma, Njombe, Katavi, Songwe na Rukwa;
Vingine ni Nzuguni (Dodoma)
katika Kanda ya Kati yenye mikoa ya Dodoma na Singida; Nyakabindi (Bariadi)
Kanda ya Ziwa Mashariki yenye mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara; Nyamuhongolo
(Mwanza) Kanda ya Ziwa Magharibi yenye mikoa ya Mwanza, Kagera na Geita; Ngongo
(Lindi) Kanda ya Kusini inayojumuisha mikoa ya Mtwara na Lindi na Fatma Mwasa
(Tabora) Kanda ya Magharibi yenye mikoa ya Tabora na Kigoma.
Akizungumza na mtandao wa
Wazo Huru Blog, Waziri huyo wa kilimo ameeleza kuwa Wakati wa sherehe hizo za
Nane Nane, Wakulima, Wafugaji, Wavuvi, Wanaushirika na Wadau wengine katika
Sekta za Kilimo; watapata fursa nzuri zaidi ya kuona na kujifunza mbinu na
teknolojia sahihi za uzalishaji na usindikaji wa mazao ya kilimo, mifugo,
uvuvi, maliasili na bidhaa nyinginezo kupitia Maonyesho ya Kilimo
yanayoandaliwa.
Aidha, kwa Wafanyabiashara
itakuwa ni fursa nzuri ya kutangaza bidhaa zao hususani pembejeo na zana
mbalimbali za uzalishaji na usindikaji wa mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na
maliasili.
Aliitaja Kaulimbiu ya
sherehe za Nane Nane Mwaka huu ni kuwa ni “Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji
wa Uchumi wa Nchi”. Kaulimbiu hii imechaguliwa baada ya kutafakari kwa
undani suala zima la Uchumi wa Viwanda unavyoweza kuchangia katika kukuza
uchumi wa mtu mmoja mmoja, pato la Taifa na wakati huo huo kupambana na
Umaskini.
"Ni ukweli ulio
dhahili kuwa Kilimo ni Sekta kubwa na muhimu kwa maendeleo kutokana na mchango
wake katika uchumi wa Taifa. Mfano katika mwaka 2017, Sekta ya Kilimo ilitoa
ajira kwa Watanzania kwa asilimia 65.5, ikichangia asilimia 28.7 ya pato la
Taifa. Sambamba na hilo Sekta ya Kilimo inachangia asilimia 65 ya malighafi za
viwandani. Takwimu zinaonesha kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2018 ukuaji
wa Sekta ya Kilimo ulifikia asilimia 7.1" Alikaririwa Mhe Hasunga
Ameongeza kuwa Kaulimbiu ya
mwaka huu inahamasisha Wakulima, Wafugaji, Wavuvi na Wanaushirika kuleta
mapinduzi katika Sekta za Kilimo kwa kuzalisha kwa tija ili kukuza uchumi wa
Mkulima, Mfugaji, Mvuvi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Kadhalika, ametoa wito kwa
Wananchi na Wadau wote kushiriki kikamilifu na kuhudhuria kwa wingi maonesho
hayo kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti, 2019.
No comments:
Post a Comment