Ofisa Habari-TTB, Geofrey Tengeneza. |
Na Suleiman Msuya
BODI ya Utalii Tanzania
(TTB), imesema itatumia Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC), kutangaza vivutio vya utalii na fursa zilizopo sekta ya utalii nchini.
Mkutano wa 39 wa SADC
unatarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 4 hadi 18/2019 ambapo Agosti 4 hadi 8/2019
itakuwa wiki ya viwanda na baadae vikao vya kitaaluma na Agosti 17 na 18
utakuwa mkutano wa viongozi wakuu wa jumuiya.
Kupitia mkutano huo
ambao unashirikisha nchi 16 wanachama wa SADC na watu zaidi ya 1,000 Rais John
Magufuli anatarajiwa kuchukua kijiti cha Uenyekiti kwa mwaka mmoja.
Serengeti National Park. |
Akizungumzia
walivyojipanga Ofisa Habari wa TTB, Geofrey Tengeneza wakati akizungumza na
Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam alisema bodi imeandaa mipango ambayo
itasaidia mkutano huo kuancha ujumbe wenye faida kwa nchi.
Tengeneza alisema TTB imeweka
mazingira rafiki ambayo yatasaidia kundi linalohusika na sekta ya utalii kunufaika
na mkutano huo hivyo kuwaomba wadau wa sekta hiyo kujitokeza na kuitumia fursa
hiyo.
“TTB tumejipanga vizuri
kwa kushirikiana na kamati ya maandalizi tumehakikisha kampuni zinazotoa huduma
ya utalii zinatumia fursa hii ya kuandaa mkutano ili na nchi inufaike kwa sasa
na baadae,” alisema.
Ofisa Habari huyo
alisema watatumia mkutano wa SADC kwa kuweka matangazo mbalimbali ndani ya
ukumbi na nje ya ukumbi, vipeperushi na kuwapatia taarifa kuhusu sektan hiyo
ili wageni wawezi kutembelea vivutio vilivyopo.
Alisema watahakikisha
wageni zaidi ya 1,000 wanatambua vivutio vilivyopo nchini kama Serengeti,
Ngorongoro, Mikumi, Ruaha, Bugiri, Katavi, Sanane, Zanzibar na kwingineko.
“Tulitoa nafasi kwa
kamapuni za utalii kuwasiliana na wageni kutoka nchi za SADC taarifa zilizopo
mwitikio ni mkubwa ambapo wapo ambao wameahidi kutembelea vivutio vyetu baada
ya mkutano na wengine wanatarajia kurudi nchini,” alisema.
Alisema iwapo mwikitio
utakuwa mkubwa kwa wageni wengi kutembelea vivutio hapa nchini itasaidia kukuza
uchumi na maendeleo nchini.
Mkutano wa SADC utashirikisha nchi 16 ambazo ni Tanzania,
Malawi, Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini, Shelisheli, Mauritius,
Angola, Comoro, Madagascar, Botswana, Eswantin, Namibia na DRC.
No comments:
Post a Comment