Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, John Kijazi, akitoa maelekezo kwa Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Joseph Bushweishaija na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Faraji
Mnyepe (kushoto), baada ya kufanya ziara ya kuangalia maandalizi ya
ukumbi wa Kimataifa Mwalimu Julius Nyerere (JNIC), utakaotumika kufanyia
mkutano wa 39 SADC. (Picha na Suleiman Msuya).
Na Suleiman Msuya
KATIBU
Mkuu Kiongozi, Mhandisi Balozi John Kijazi ameitaka Kamati ya Maandalizi ya
Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kuhakikisha
maandalizi yanakamilika kwa asilimia 100 kabla ya mikutano kuanza Agosti 4/2019.
Aidha,
Kijazi amewaomba Watanzania kutumia fursa ya mkutano wa SADC kufanyika nchini
kuchochea uchumi wa Tanzania.
Katibu
mkuu aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya
kumaliza ukaguzi wa Ukumbi Julius Nyerere International (JNIC) utakaotumika
kwenye mkutano huo kuanzia Agosti 4 hadi 18 mwaka huu.
Alisema
amezunguka na kujinea ambapo maandalizi yanaenmdelea vizuri na kuitaka kamati
kuongeza kasi ili kila kitu kikamilike ndani ya muda uliopangwa.
Balozi
Kijaji alisema Tanzania inatakiwa kuonesha nchi wanachama wa SADC kuwa inaweza
kufanya mambo makubwa hivyo maandalizi mazuri ni muhimu.
“Nimeona
maandalizi yapo vizuri ila nitumie nafasi hii kuipa kamati ikamilishe kwa
wakati kama ambavyo tumekubaliana,”alisema.
Alisema
mkutano huo unatarajiwa kumkabidhiri Rais John Magufuli Uenyekiti wa SADC hivyo
unapaswa kutumika vizuri ikiwemo maandalizi maziru ya mkutano huo.
Kijazi
alisema mkutano huo utaanza Agosti 4 hadi 8/ 2019 kwa wiki ya viwanda ambapo
zaidi ya washiriki 1,000 kutoka nchi wanachama wanatarajiwa kuonesha shughuli
wanazofanya.
Pia
alisema baada ya wiki ya viwanda kutakuwa na mikutano ya kitaalam, makatibu
wakuu, mawaziri na Agosti 17 hadi 18/2019 utakuwa mkutano wa viongozi wakuu wa
SADC.
Aidha,
Balozi Kijazi amewaomba Watanzania kutumia mkutano huo kama fursa ya kiuchumi ili
kuweza kuisukuma Tanzania katika uchumi wa viwanda.
Balozi
alisema mkutano wa SADC utahitaji wafanyabiashara, wasafirishaji, wenye
mahoteli, sekta ya utalii na nyinginezo hivyo Watanzania wanapaswa
kuzichangamkia.
Katibu
mkuu kiongozi aliwaasa waandishi wa habari nchini kutumia kalamu zao vizuri kwa
kuandika mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ili nchi za SADC ziweze
kujifunza na kunufaika.
Alisema
Tanzania ina historia ndefu kwa nchi za SADC hivyo ni wajibu wa waandishi wa habari
kuandika mema ambayo yamefanywa ili kuendelea kuitangaza nchi.
Mkutano
wa SADC utashirikisha nchi 16 ambazo ni Tanzania, Malawi, Msumbiji, Zambia,
Zimbabwe, Afrika Kusini, Shelisheli, Mauritius, Angola, Comoro, Madagascar,
Botswana, Eswantin, Namibia na DRC ambapo zaidi ya washiriki 1,000 wanatarajiwa
kushiriki.
No comments:
Post a Comment