NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI imetoa wito kwa
wadau wa elimu kushirikiana na Serikali katika kujenga mazingira mazuri ya
utoaji wa elimu nchini ikiwemo ujenzi wa madarasa, vyoo na nyumba za walimu.
Kauli hiyo imetolewa leo
mjini Mwanza na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) - anayeshughulikia Elimu Tixon Nzunda wakati wa ufunguzi wa
kikao kazi cha kuandaa vipindi vya redio kupitia Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (MKUE-Tanzania)
Alisema hali ilivyo sasa ili
kukamilisha miundombinu na kuweka mazingira mazuri ya utaoji wa elimu na ujenzi
wa nyumba za kuishi walimu zinahitajika shilingi trilioni 14 kutekeleza zoezi
hilo katika Shule za Sekondari na Msingi nchini kote.
Nzunda alisema Serikali
pekee yake haiwezi kukamilisha zoezi hilo bila kushirikiana na wadau wengine ili
kujenga madarasa ya kutosha ili kupunguza msongamano wa wanafunzi, kuondioa uhaba
wa nyumba za walimu na vyoo.
Alisema Serikali katika
kukabiliana na tatizo la msongamano wa wanafunzi katika shule mbalimbali za
Msingi na Sekondari tayari katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita imetoa
zaidi ya bilioni 65 kwa ajili ya ujenzi wa maboma ya madarasa 5,289 nchini kote.
Nzunda alisema kuwa fedha hizo zimesaidia kukamilisha maboma 2,392
kwa ajili ya Sekondari na 2,897 ni kwa
ajili ya Msingi nchini kote.
Aidha Naibu Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) -
anayeshughulikia Elimu aliwataka wadau wa elimu ikiwemo
Alisema kuwa badala ya
Asasi zisizo za Kiserikali(NGOs) kutumia
fedha katika utetezi(advocacy) unaonyesha na kutangaza changamoto na mapungufu katika
Shule nchini kama vile msongamano na upungufu wa matundu ya vyoo mashuleni ni
vema wakatumia fedha hizo kushirikiana na Serikali katika kuboresha mazingira
ya Shule nchini.
Katika hatua nyingine Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) -
anayeshughulikia Elimu amepiga marufuku kwa walimu wanaofundisha madarasa ya kuanzia elimu ya awali hadi darasa
la tatu kuingia na viboko madarasa.
Alisema kuwa vitendo hivyo
vinasababisha wanafunzi wa madarasa hayo kuogopa na kutokuwa wasikivu wakati wa
wanapofundishwa.
Kuhusu Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (MKUE-Tanzania) alisema
kuwa umechangia katika kuboresha elimu katika mikoa 9 kiwango cha ufaulu kwa
shule za Msingi umeongezeka kutoka chini asilimia 40 hadi kuwa juu ya 77 na maeneo mengine kufikia asilimia 100.
Mafunzo hayo ya siku tatu
kupitia Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (MKUE-Tanzania) yanayowashirikisha
waandishi wa habari, Maafisa Elimu Mikoa na Maafisa Habari kutoka Mikoa 9
yameandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya
Kimataifa ya Uingereza(DFID)
No comments:
Post a Comment