Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa Meneja Mawasiliano wa Asasi inayolenga kutokomeza Ukimwi kwa watoto na familia,(AGPAHI), mwanahabari Agnes Kabigi, wakati wa kuaga mwili wake Kahama mkoani Shinyanga, kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa mazishi. (Picha na Malunde Blog).
Mfanyakazi wa AGPAHI Mkoa wa Shinyanga, Kasablankhahr Herman, akizungumza wakati wa kuaga mwili wa marehemu Agnes Kabigi.
Mfanyakazi wa AGPAHI Mkoa wa Shinyanga, Kasablankhahr Herman, akizungumza wakati wa kuaga mwili wa marehemu Agnes Kabigi.
Kahama, Shinyanga
Mwili wa Meneja Mawasiliano wa asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Bi. Agnes Kabigi umeagwa leo Jumamosi Julai 27,2019 Mjini Kahama mkoani Shinyanga na kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi.

Agnes Kabigi alifariki dunia jana mchana Ijumaa Julai 26,2019 baada
kuanguka ghafla wakati akitekeleza majukumu yake akiwa katika Hospitali
ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Agnes Kabigi ni mwandishi Mwandamizi aliyewahi kufanya kazi katika
Magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Nipashe na mpaka umauti unamkuta alikuwa
anafanya kazi katika Shirika la AGPAHI linalojihusisha na mapambano
dhidi ya VVU na UKIMWI ambalo linafanya kazi zake katika mikoa ya
Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa shirika la AGPAHI,wakati wa kuaga
mwili wa marehemu, Mfanyakazi wa AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Kasablankhahr
Herman amesema mwili wa Agnes utasafirishwa kwa ndege majira ya saa 10
leo jioni kutoka Mwanza hadi Jijini Dar es salaam kwa ajili ya mazishi.
Agnes alizaliwa tarehe Julai 13,1967.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Agnes Kabigi. Amina
No comments:
Post a Comment