*Ataka wawe na
mipango kazi, asema Serikali inapima matokeo
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiongea na Viongozi na Watumishi
wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, katika ukumbi wa Halmashauri Julai 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua darasa lililokarabatiwa la
Shule Kongwe ya Same Sekondari, mkoani Kilimanjaro Julai 19.2019. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Same Sekondari Hoza Mgonja.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua maabara katika Shule
Kongwe ya Same Sekondari, kabla ya kuzindua mradi wa ukarabati wa shule hiyo
kongwe, mkoani Kilimanjaro Julai 19.2019.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia darasa lililokarabatiwa
la Shule Kongwe ya Same Sekondari, katika mradi wa ukarabati wa shule hiyo
kongwe mkoani Kilimanjaro, Julai 19.2019.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia vitabu katika maktaba iliyokarabatiwa
ya Shule Kongwe ya Same Sekondari, katika mradi wa ukarabati wa shule hiyo
kongwe mkoani Kilimanjaro, Julai 19.2019. Kushoto ni Mwalimu Mkuu
wa Shule ya Same Sekondari Hoza Mgonja.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua mradi wa ukarabati wa
shule kongwe ya Same Sekondari, iliyoko wilayani Same katika mkoa wa Kilimanjaro, Julai 19.2019.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wanafunzi wa Same Sekondari mara baada ya kuzindua mradi wa ukarabati wa shule hiyo kongwe, iliyoko
wilayani Same katika mkoa wa Kilimanjaro, Julai 19.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza mwanafunzi wa Same Sekondari, Omari
Pundugu, akielezea changamoto mafanikio na changamoto za shule hiyo mara baada
ya uzinduzi wa mradi wa ukarabati wa shule hiyo kongwe,
iliyoko wilayani Same katika mkoa wa Kilimanjaro, Julai 19.2019.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasalimia wananchi, baada ya
kuzindua mradi wa ukarabati wa shule kongwe ya Same Sekondari, mkoani Kilimanjaro Julai 19.2019.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa
umma wawe na mipango ya kazi ambayo itaweza kupimika na kutoa matokeo.
“Kila mtumishi anapaswa awe na mpango kazi katika
sekta yake na ni lazima aende kupima matokeo. Awamu hii, tunataka kuona matokeo
ya kazi zenu."
Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Ijumaa, Julai 19,
2019) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Same kwenye ukumbi wa
Halmashauri ya wilaya hiyo, mjini Same.
“Watumishi mmeletwa kwenye wilaya hii ili
muwahudumie wananchi. Tulioajiriwa, kazi yetu kubwa ni kuwatumikia wananchi
bila ubaguzi wowote uwe ni wa kabila, itikadi au rangi.”
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha
watumishi hao kwamba baada ya mchujo wa watumishi hewa, waliobakia wanapaswa
kufanya kazi kwa bidii.
"Fanyeni kazi kwa bidii, msimamo wa Serikali hii
ni kwamba hatumvumilii mtumishi ambaye si mwajibikaji, ni mwizi, mzembe au
anaomba rushwa. Serikali hii hatuna muda wa kujadili matatizo ya watumishi,
tunamalizana hapo hapo," amesema.
Amewataka watumishi hao wasimamie utekelezaji wa
ahadi zilizotolewa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi kwa sababu
ndiyo chama tawala.
"Mtumishi angalia sekta yako inasema nini,
ifanyie kazi. Kama ni maji, tafuta ni wapi yanapatikana, changanua zinahitajika
shilingi ngapi, tafuta njia ya kupata hizo fedha ili wananchi wapate
maji."
Kuhusu tabia ya kukaa ofisini, Waziri Mkuu amekemea
tabia hiyo na kuwataka watumishi wote nchini waache tabia ya kukaa ofisini na
badala yake waende vijijini kuwasikiliza wananchi.
"Watumishi wa umma msikae ofisini. Nendeni
vijijini walau kwa siku nne za juma. Hizo mbili zinazobakia, zitumieni kuandaa
taarifa. Nendeni huko ili wananchi wasipate usumbufu wa kuja hapa mjini
kuwatafuta," amesisitiza.
"Mkuu wa Wilaya simamia zoezi la wakuu wa idara
na wasaidizi wao kwenda vijijini. Wakienda vijijini ni lazima waonane na
waheshimiwa madiwani, washirikiane kusikiliza kero na kutafuta majibu kwa
wananchi. Huo ndiyo mshikamano wenyewe unaohitajika," amesema.
Wakati
huohuo, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma watambue mipaka yao na wajenge
mahusiano baina yao na wengine.
Alitoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Julai 18,
2019) wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Moshi, kwenye ukumbi wa
mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
"Kila mmoja lazima atambue mipaka yake na
mamlaka baina yake na wengine. Hapa mko wateuliwa, waajiriwa na
wachaguliwa. Kila mtu ana nafasi yake ya kuwatumikia wananchi.
Aliwataka watumishi hao watambue falsafa ya Kiongozi
mkuu wa nchi ambayo inahimiza uchapakazi. “Kwa hiyo tunaposema Hapa
Kazi Tu, maana yake
chapa kazi na tuone matokeo. Tunasisitiza kazi na tunataka kazi unayoifanya,
itoe matokeo,” alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI
MKUU,
IJUMAA, JULAI 19,
2019.
No comments:
Post a Comment