HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 27, 2019

BARABARA YA KISONGO BYPASS KUFUNGUA FURSA ZA KIUSALAMA UWANJA WA NDEGE ARUSHA

Mhandisi wa jiji la Arusha August Mbuya akitoa maelezo leo kwa Kaimu Mkurugenzi wa jiji hilo, Sifael Kalanga, kabla ya makabidhiano ya barabara ya Kisongo Bypass kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa Mkandarasi Kampuni ya Snohydro kutoka China. (Picha na Ahmed Mahmoud Arusha).
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro, akipata maelezo kutoka kwa mhandisi wa jiji la Arusha August Mbuya katikati mwenye kikoti akiwa na Kaimu mkurugenzi wa jiji la Arusha Sifael Kulanga wakati wa makabidhiano ya barabara kwa Kampuni ya Snohydro ambaye ndiye Mkandarasi wa ujenzi wa barabara ya kilomita 3.442 itakayogharimu kiasi cha billion 4.106 hadi kukamilika Januari 2020.

Picha ya pamoja.
Tukio la makabidhiano hayo kati ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Arusha Sifael Kulanga na Mhandisi wa barabara wa kampuni ya Snohydro Lang Shang kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hiyo ya Kisongo bypass nje kidogo ya jiji la Arusha eneo la Kata ya Olasit jijini Arusha.Mhandisi wa barabara kutoka Kampuni ya Snohydro Lang Shang (kushoto), akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Arusha Sifael Kulanga wakipata maelezo kwenye tukio la makabidhiano ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Kisongo Bypass nje kidogo ya jiji la Arusha eneo la kata ya Olasit.

Na Ahmed Mahmoud, Arusha

Halmashauri ya Jiji la Arusha limepata Fedha za nyongeza kiasi cha bilion 4,106 kwa ajili ya ujezi wa barabara ya kisongo Bypass yenye urefu wa kilometa 3.44 kupitia fedha za mradi wa TSCP inayoratibiwa na benki ya dunia chini ya Ofisi ya Rais Tamisemi

Mradi huo ambao tarehe 27 mwezi huu umekabidhi na Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa Mkandarasi Kampuni ya Ujenzi ya Snohydro ya nchini china utatekelezwa kwa muda wa miezi minne hadi Januari mwakani.

Akizungumza mara baada ya kuukabidhi mradi huo kwa kampuni hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Sifael Kulanga ambaye pia ni Mwanasheria wa jiji hilo amesema kuwa mradi huo ni wanyongeza na utatekelewa ndani ya miezi minne.

Alisema kuwa mradi huo utasaida sana kuondoa changamoto za msongamano katikati ya jiji la Arusha na una manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi na utasaidia usalama kwenye uwanja mdogo wa ndege badala ya kukata katikati ya uwanja barabara hiyo itasaidia kuchepuka pembezoni mwa uwanja.

“Barabara hii ina umuhimu mkubwa sana katika uwanja wetu wa ndege na maeneo ya shule ya sekondari na itafungua fursa kwa wanaowahi katikati ya jiji kutoka stand kubwa ya mabasi ya mkoani inayotarajiwa kujengwa Olasit”

Kwa upande wake Mhandisi wa barabara wa kampuni ya Snohydro watakaojenga barabara hiyo Lang Yang Shang alisema kuwa wataifanya kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa na kwa viwango vilivyowekwa na kwa ubora.

Alisema kuwa barabara hiyo na udogo ulipo hautawapa tabu kuikamilisha ndani ya wakati hivyo kuweza kukamilika bila kuwepo vikwazo vyovyote hivyo kuomba ushirikiano wakati wote wa ujenzi huo.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo Mhandisi Agustini Mbuya alisema kuwa barabara hiyo ni muunganiko wa bypass na itarahisisha mchepuko na kusaidia usalama na kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutenga fedha hizo.

Alisema kuwa mradi huo utaanza ujenzi rasmi tarehe 11 mwezi ujao na leo ndio makabidhiano kwa jiji kumkabidhi rasmi mkarandari kwa ajili ya Ujenzi huo wa barabara

Nae Mstahiki meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro alisema kuwa Barabara hiyo ni sehemu ya mkataba uliosainiwa wiki iliyopita na utakuwa kielelezo cha kueleza jinsi utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa wananchi mwaka ujao jinsi serikali ilivyotekeleza miradi.

No comments:

Post a Comment

Pages