Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, akizungumza na wafanyakazi wa
NMB kwenye banda la benki hiyo wakati wa uzinduzi wa maonesho ya nanenane
katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, akizungumza na wafanyakazi wa
NMB kwenye banda la benki hiyo wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Nanenane
katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (wa pili kushoto) akitazama
Bidhaa za mfanyabiashiara Raphael Buja (Buja Pure Honey) kwenye banda la NMB,
wakati wa uzinduzi wa maonesho ya nanenane katika viwanja vya Nyakabindi mkoani
Simiyu, kushoto ni Meneja Mwandamizi Biashara na Kilimo wa NMB John Mchunda,
Mkuu wa Idara ya biashara kwa Serikali kutoka NMB Vicky Bishubo (aliyevaa
skafu).
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (wa pili kushoto) akitazama
Bidhaa za mfanyabiashiara Raphael Buja (Buja Pure Honey) kwenye banda la NMB,
wakati wa uzinduzi wa maonesho ya nanenane katika viwanja vya Nyakabindi mkoani
Simiyu, kushoto ni Meneja Mwandamizi Biashara na Kilimo wa NMB John Mchunda,
Mkuu wa Idara ya biashara kwa Serikali kutoka NMB Vicky Bishubo (aliyevaa
skafu).
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kuwa wakati
serikali ikijiandaa kufanya marekebisho makubwa ya sera ya kilimo, taasisi
za kifedha nchini zitajumuishwa katika kutoa maoni jinsi gani zinaweza
kushiriki kikamilifu kwenye kilimo.
Alisema kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo imepanga kuweka
mazingira rafiki kwa taasisi za kifedha ili ziwekeze kwenye sekta hiyo, ikiwa
pamoja na kuangalia mfumo gani sahihi wa utolewaji mikopo kwa wakulima.
Naibu Waziri huyo ameyasema hayo jana wakati alipotembelea banda
la Benki ya NMB kwenye maonyesho ya sikuu ya wakulima kitaifa (Nanenane)
yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Alisema kuwa kumekuwepo na tatizo la pembejeo hasa kwenye kilimo
cha pamba, ambapo serikali kupitia bodi ya pamba imekuwa ikitumia fedha nyingi
kuziagiza na kupelekwa kwa wakulima lakini matokeo yamekuwa hayaonekani.
“Nitakutana na taasisi zote za fedha tufanye majadiliano kwenye
sera mpya wa kilimo wao wanaweza vipi kushiriki moja kwa moja mpaka kwa
wakulima, wanaweza vipi kuweka mfumo mzuri na rahisi wa kutoa mikopo kwa
wakulima wa chini,” alisema Bashe.
“ Tunahitaji benki zihusike katika kubadilisha mfumo wa kuagiza
pembe nje, tuache kutumia mawakala na baadala yake twende moja kwa moja
viwandani kwa kutumia fedha zao na zitarejeshwa na wakulima mara baada ya
kuvuna,” aliongeza Bashe.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Biashara za serikali Vicky
Bishubo kutoka NMB alisema kuwa taasisi za kifedha kujumuishwa kwenye
marekebisho ya sera hiyo ni suala muhimu.
Alisema NMB kupitia kilimo biashara (Agri-business) utakuwa
wakati sahihi katika kuhakikisha wakulima na wajasliamali nchini wanawezeshwa
zaidi kupitia vikundi vyao ili waweze kuongeza tija katika uzalishaji.
Aliongeza kuwa NMB inatambua kuwa inalo jukumu kubwa la
kuhakikisha wakulima na wananchi wote maeneo ya vijini, wanajumuishwa katika
mfumo rasmi wa fedha kupitia kupewa elimu na mafunzo.
Naye Meneja Mwandamizi katika mahusiano ya biashara ya kilimo
kutoka NMB, John Mchunda alisema kuwa
benki hiyo ilitenga kiasi cha sh. Bilioni 500 kwenye kilimo- biashara kwa
muda wa miaka mitano toka mwaka 2015 kwa ajili ya kusaidia mnyororo wa thamani kwenye
sekta ya kilimo na wakulima wenyewe. Na baada ya fedha hizo kuisha mwaka jana,
NMB imeongeza bilioni 500 nyingine kusaidia kukuza mnyororo wa thamani (Agricultural
value Chain) kwa wakulima, Wafugaji na wavuvi na biashara zao.
No comments:
Post a Comment