Meneja Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, Godluck
Shirima, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuelezea ushirikiano wao
katika Maonesho ya Nne Wiki ya Viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini
mwa Afrika (SADC), yanafanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Suleiman
Msuya).
NA SULEIMAN MSUYA
NA SULEIMAN MSUYA
KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imesema katika mwaka 2018/2019 itatoa gawiwo la shilingi milioni 22 kwa wanahisa wake.
Aidha,
kampuni hiyo imetoa shilingi milioni 300 kufadhili Mkutano wa 39 wa
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ulionza jana jijini Dar
es Salaam.
Hayo yamesemwa
na Meneja Sheria na Uhusiano ya Kampuni, Godluck Shirima wakati
akizungumza na waandishi wa habari baada ya Rais John Magufuli
kutembelea banda la Puma lililopo katika maonesho ya. Nne ya Wiki ya
Viwanda ya SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Shirima
alisema Kampuni ya Puma imekuwa ikifanya vizuri mwaka hadi mwaka hivyo
kuamua kuendelea kutoa gawiwo kwa wanahisa baada ya kuondoa gharama za
usimamizi na miradi ya kijamii.
Meneja
huyo alisema katika gawiwo hilo la shilingi bilioni 22 Serikali ambayo
ina asilimia 50 ya Hisa itapata shilingi bilioni 11 na Puma bilioni 11.
Alisema
kiasi hicho ni cha gawiwo ni ongezeko la bilioni 2 za mwaka 2017/2018
kwa kila mwana hisa ambapo gawiwo lilikuwa shilingi bilioni 18.
"Tunamuomba
Rais atupe nafasi ili tuende kumkabidhi wenyewe gawiwo la shilingi
bilioni 11 ambalo tunapaswa kuipata Serikali naamini mwakani
litaongezeka," alisema.
Aidha,
Shirima alisema ongezeko la gawiwo hilo linatokana mazingira mazuri ya
kibiashara na uwepo wa miradi mikubwa yenye tija kwa nchi.
Alisema
Puma imeweka mfumo wa mafuta katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) na kutoa mafuta ujenzi wa Daraja la Salendar hivyo
matumaini yao ni kupitia miradi hiyo mikubwa wataongeza gawiwo.
Kuhusu
ufadhili wa mkutano wa SADC, Shirima alisema Kampuni ya Puma inafanya
kazi na nchi 13 wanachama hivyo imeona irudishe fadhila kwa kuwa
wadhamini wakuu.
Shirima
alisema Kampuni ya Puma itaendelea kushirikiana na nchi wanachama wa
SADC ili kuhakikisha dhamira ya nchi hizo kufikia uchumi wa viwanda
inatimia.
Awali Rais
Magufuli akitembelea mabanda aliipongeza kampuni hiyo kwa kazi nzuri
wanayofanya na kusisitiza ushirikiano baina yao na Serikali.
No comments:
Post a Comment