Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kagera, Denice Michael Kunyanja.
Na Lydia Lugakila, Kagera
Madreva waendesha pikipiki maarufu
kama bodaboda mkoani Kagera wametajwa kushughulikiwa vikali kutokana na kukiuka
baadhi ya sheria za usalama barabarani
hasa matumizi mabaya ya alama ya Zebra kutokana na mwendo kasi jambo linalosababisha
ajali kwa watembea kwa miguu.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kagera, Denice Kunyanja, wakati
akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa.
Kunyanja amesema kuwa kuna baadhi ya
Madreva pikipiki maarufu kama Boda boda hawafuati sheria na kanuni za
barabarani ikiwemo kuendesha vyombo vyao
kwa mwendo kasi, kutowaheshimu watembea kwa mguu wanaposimama katika alama ya
zebra jambo linalosababisha ajali kila kukicha.
kutokana na hali hiyo kamanda huyo amesema tayari
wamejipanga ili kuhakikisha tabia hiyo inakoma mara moja kwa madreva hao kwa kuwachulia sheria kali ikiwemo
kutiwa mbaroni.
Kunyanja Ametaja kundi la watembea kwa miguu
ambao ni Waathilika wakubwa kwenye
vivuko ni wazee, watoto na watu wenye ulemavu.
Amesema kuwa baadhi ya
Madreva wamekuwa na tabia isiyofaa pale wanapofika sehemu za alama ya zebra
hawawaheshimu watembea kwa miguu wanapokuwa
katika eneo la kivuko wakati
mwingine pikipiki zao hupalamia magari ambayo yamesimama pembezoni mwa
barabara.
Kamanda Kunyanja Amesema kuwa elimu
juu ya usalama barabarani itaendelea kutolewa huku zoezo la ukamataji kwenye zebra likiendelea.
Hata hivyo ametoa wito kwa madreva hao
kuwaheshimu watembea kwa miguu na kuiheshimu sehemu ya alama ya zebra kwani ni sehemu pekee
ambayo mtembea kwa miguu anatumia na kuwa Kila mtu aheshimu uhai wa mtu kwa kutii sheria
za usalama barabarani na kudai kuwa watumia barabara hawajajua
umuhimu wa kutumia alama za Barabarani
hata na watembea kwa miguu wanatumia Barabara ndivyo hivyo.
No comments:
Post a Comment