Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia akisisitiza jambo kwa Msimamizi wa Mradi wa Tanga Uwasa Mhandisi Shame Juma katikati wakati alipotembelea eneo la Bwawa ambalo litatoa maji kupelekea kwa wananchi eneo la Horohoro mpakani mwa Tanzania na Kenya mradi huo unaotekelezwa na mamlaka hiyo utakapomalika kushoto ni Msimamizi wa Mtandao wa Maji Tanga Uwasa George Mbalai.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia jambo kwa Msimamizi wa Mradi Tanga Uwasa Mhandisi Shame Juma wakati alipotembelea na kukagua eneo ambalo kutajengwa kituo kusafisha maji kabla ya kusambaza kwa wananchi pamoja na kituo cha Forodha kinachounganisha nchi ya Tanzania na Kenya kilichopo eneo hilo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akiwa na watumishi wa mamlaka hiyo wakitazama eneo ambalo kutajengwa kituo cha kusafishia maji kabla ya kwenda kwa wananchi eneo la horohoro.
Na Mwandishi Wetu
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly wakati alipotembelea na kukagua bwawa la maji eneo hilo wakati wa makabidhiano ya mabomba 415 yenye thamani ya milioni 64.4 yatakayotumika kwenye mradi huo kwa uongozi wa serikali ya Kijiji cha Horohoro.
Alisema kwamba mradi huo ambao utakuwa ni kutoa maji kwenye chanzo cha maji ambao ni bwawa na kupelekwa kwenye tenki ambalo litakarabatiwa na kusambazawa kwa wananchi pamoja na kituo cha Forodha Horohoro ili kuweza kuondosha kero ya maji kwa wananchi.
Licha kutembelea bwawa hilo lakini pia alifika eneo ambako kunaendelea kujengwa kituo cha kusafishia maji kabla ya kuwafikia wananchi wanaoishi eneo hilo la mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mhandisi Hilly alisema kwamba alisema mamlaka hiyo wamepewa kazi na wizara ya maji kwa ajili ya kujenga mradi huo ambao utasaidia kuondosha shida ya maji.
Alisema kwamba hilo linatokana na eneo hilo kuwepo kwa ukosefu mkubwa wa maji licha ya kuwa na bwawa ambalo lina uwezo wa kuhifadhi maji lakini wanapata maji yasiyo salama kwa matumizi ya binadamu
Alisema kwamba mabomba hayo ni hatua mojawapo ya ujenzi mradi wa maji Horohoro kwa ajili ya kusafisha maji na kusambaza kwa wananchi pamoja na kituo cha Forodha kinachounganisha nchi ya Tanzania na Kenya kilichopo eneo hilo.
Aidha alisema kwamba sambamba na ujenzi huo lakini pia watawekwa vituo vidogo vya kuchotea maji (vioski) huku akieleza kwa mujibu wa takwimu za watendaji kwamba wananchi 5000 wanaishi maeneo hayo ndio watanufaika.
“Lakini pia mradi huu utakapokamilika utakuwa mkombozi mkubwa sana kwa wananchi lakini hata watumishi waliopo eneo la mpakani kwani walikuwa wanapata changamoto ya maji safi ikiwemo TRA kutokana na maji kutokuwa salama walikuwa wakifuata maji Tanga mjini na kuyatumia kwenye ofisi zao “Alisema
Awali akizungumza wakati wa halfa ya upokea wa mabomba hayo Mwenyekiti wa Kijiji cha Horohoro Kata ya Duga Maforoni wilayani Mkinga mkoani Tanga Miliya Merieyer alisema kabla ya mradi huo changamoto ya maji ilikuwa kubwa sana kutokana na kulazimika kufuata maji kwenye mto Umba uliopo nchini Kenya.
Alisema kwamba licha yam to huo kutokea nchini Tanzania lakini ukifaka maeneo hayo unaingia kwenye nchi hiyo sasa ilikuwa wanatembea kilomita 8 kutoka mpakani hadi huko watu walikuwa wakinunua maji 500 hadi 1000 lakini alipochaguliwa 2015 ndio akaanza kuhangaikia suala hilo.
Alisema kwamba kulikuwa na bwawa hilo ambalo lilikuwa limechimbwa na watu wa TASAF lakini wakalitelekeza ikawa ikinyesha mvua maji yanapita na hivyo kukutana na wananchi kutaka kulitengeneza na kuziba eneo lililokwa likivuja mvua iliponyesha watu walikuwa wakichota maji walipoona maji yanazidi kujaa akalazimika kwenda wilayani kuomba fedha akaambiwa hawana fedha.
Alisema baadae aliomba Mhandisi wa maji wilayani kufika eneo hilo ili aweze kuwafanyia mahesabu ili waweze kuona namna ya kupambana kuhakikisha wanasaka vifaa vya kutoa maji kwenye chanzo hicho huku akieleza kutokana na juhudi hizo aliweza kupata mabomba ambayo yaliwaweza kupata maji kutoka bwawani mpaka kwenye meneo ya karibu wananchi wakafurahi na kuamua kuuza maji hayo kwa sh.100 mpaka kufikia milioni 6.
Akizungumza adha ya maji waliokuwa wakikumbana nayo eneo hilo alisema suala hilo lilikuwa kama mtaji wa mtu kwamba wanatoa maji Tanga mjini hadi Horohoro kwenda kuwauzia wananchi.
Hata hivyo alisema kwamba baada ya waziri alivyokuja kukagua bwawa hilo akakuta maji yapo akwaambia wanaweza kuwaboreshea bwawa hilo baada ya waziri kuondoka wahandisi wakaanza kwenda eneo hilo na kuhaidi kupelekea mabomba huku ujenzi wa kituo cha kusafishia maji ukianza kujengwa.
“Kwa kweli niishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt Magufuli tulilia muda mrefu msaada wa maji lakini halikuweza kufanikishwa lakini Waziri Mbarawa alivyokuja wakaaona kama ni stori za miaka ya nyuma lakin mambo yamekuwa tofauti tunaona jambo hili linashughulikiwa kwa vitendo “Alisema
No comments:
Post a Comment