HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 10, 2019

Benki ya CRDB yawakumbuka wakandarasi, watoa huduma

 Ofisa Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dk. Joseph Witts, akizungumza na wakandarasi na watoa huduma wanaoshiriki ujenzi wa miradi miwili mikubwa ya uzalishaji Umeme katika Mto Rufiji Nyerere Hydropower pamoja na ujenzi wa Reli ya Kisasa 'SGR' inayotekelezwa na serikali. (Picha na Francis Dande).

Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), Rhoben Nkori, akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wakandarasi na watoa huduma katika miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali.
Ofisa Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dk. Joseph Witts, ambaye alikuwa mgeni rasmi (kushoto) akiwa na baadhi ya maofisa kutoka Kampuni ya Yerpi Merkez, mkandarasi mama wa ujenzi wa reli ya umeme 'Standard Gauge Railway Project'.

Meneja wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Claudia William, akitoa mada.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo.

Mkuu wa kitengo cha Biashara Benki ya CRDB, Toyi Ruvumbagu, akitoa mada katika mkutano uliowakutanisha wakandarasi na watoa huduma katika miradi mikubwa ya serikali.

Mkurugenzi wa Masuala ya Kampuni Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, akizungumza katika mkutano huo.





Mmoja wa washiriki Bw. Severine akiuliza swali.





Mmoja wa wateja wa Benki ya CRDB, Bi. Hawa akiuliza swali katika mkutano huo.

Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa, akijibu maswali ya wateja wa benki hiyo. Meneja Mikopo kwa Wajasiriamali Wanawake wa Benki ya CRDB, Rehema Shambwe (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB) Mhandisi Consolata Ngimbwa.


NA MWANDISHI WETU

BENKI ya CRDB imefungua milango kwa wakandarasi na watoa huduma wazawa wanaoshiriki ujenzi wa miradi miwili mikubwa inayotekelezwa na Serikali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam alipokutana na wakandarasi hao, Ofisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk. Joseph Witts, alisema benki hiyo inalenga kuongeza ufanisi kwenye miradi hiyo.

Witts aliitaja miradi ambayo wakandarasi na watoa huduma wake watapewa mitaji ili kufanikisha shughuli zao ni ule wa umeme kutoka mto Rufiji ulipewa jina la Nyerere Hydropower na ule wa reli ya umeme.

Kwa mujibu wa Witts, uongozi wa benki hiyo umeona ipo haja ya kukutana na wakandarasi na watoa huduma wanaofanya kazi kwenye miradi hiyo ili kuwaongezea ufanisi kwa kuboresha mitaji yao na kuharakisha kukamilika kwa miradi hisika.

Alisema mapema mwaka huu, benki ya CRDB ilitoa uwezeshaji wa Dola milioni 20 za Marekani na malipo ya awali ya Dola milioni 88 kwa Kampuni ya Yerpi Merkez, mkandarasi mama wa ujenzi wa reli ya umeme 'Standard Gauge Railway Project'.

"Benki ya CRDB pia imetoa kiasi cha Dola milioni 221 kama mkataba wa malipo ya awali ya kusaidia ujenzi wa mradi wa umeme kwenye Mto Rufiji uliopewa jina la Baba wa taifa Mwalimu Nyerere kwa mkandarasi mkubwa kampuni ya JV Arab na Elsewedy Electric.

"Tumelenga kuwathaminisha wakandarasi na watoa huduma kwenye miradi hii waliopo katika mnyororo wa thamani baada ya kutoka kwa wakandarasi wakubwa tutawasaidia kufanikisha shughuli zao zote," alisisitiza Witts.

Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi, Rhoben Nkori, aliishukuru benki ya CRDB kwa kuiona changamoto ya utekelezaji wa kazi kwa wakandarasi na watoa huduma wadogo huku akiahidi ufanisi na kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati.

No comments:

Post a Comment

Pages