Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiangalia mmoja wa faru weusi kati ya faru tisa ambao wapo kwenye banda maalum mara baada ya kushushwa kwenye ndege mara baada ya kuwasili leo katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro wakiwa wametokea nchi ya Afrika Kusini. Faru hao wameletwa nchini ili kuja kuongeza idadi ya faru waliopo kutokana vitendo vya ujangili kushamiri Sikh za nyuma . Wengine ni baadhi ya viongozi Taasisi za uhifadhi nchini pamoja na Wakuu wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Na Mwandishi Wetu
Serikali ya Tanzania imepokea faru weusi tisa kutoka nchi ya Afrika ya Kusini ambao watapelekwa katika Hifadhi mbalimbali nchini.
Faru
hao wamepokelewa leo Septemba 10, 2019 na Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa pamoja na viongozi mbalimbali
katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro( KIA)
Akizungumza
mara baada ya kupokea faru hao, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe.Constantine Kanyasu amesema tukio hilo ni la kihistoria kwa vile ni
mara ya kwanza kupokea idadi kubwa ya faru kwa wakati mmoja.
Hata
hivyo, Mhe.Kanyasu amesema idadi ya faru hao walikuwa kumi ambapo
faru mmoja kati ya hao kumi alipoteza maisha wakati akiwa njiani
kuletwa nchini.
Mhe.Kanyasu amesema faru hao
watalindwa kwa gharama yoyote ile ili kuhakikisha hawapungui kama
ilivyotokea katika miaka 1970-1980.
Amesema
tatizo la ujangili ndiyo sababu kuu iliyopelekea kupungua kwa faru hali
iliyopelekea maeneo mengine katika nchi faru hao kutoweka kabisa na
sasa imebaki historia.
Aidha, Mhe.Kanyasu
ametoa wito kwa jamii pamoja na Wahifadhi kuwa Wazalendo kwa kuwalinda
faru hao ambapo kwa sasa Serikali inafanya jitihada ya kuzuia wasiweze
kutoweka kabisa.
Katika hatua nyingine,
Mhe.Kanyasu amewashukuru Wadau wa Uhifadhi nchini hususan Uongozi wa
Mfuko wa Grumet kwa jitihada kubwa za kuwezesha upatikanaji wa faru hao.
Amesema
hadi hivi sasa jitihada mbalimbali ambazo zilichukuliwa na Serikali
kwa kushirikiana na Wadau wa Uhifadhi nchini katika miaka ya 90
zimeanza kuzaa matunda katika Hifadhi nchini.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Grumeti amesema wayaendelea
kushirikiana na Serikali mikakati yenye maslahi kwa Taifa katika
kuhifadhi wanyamspori
Ameeleza kuwa ujio wa faru hao ni hao ni utekelezaji wa kuongez idadi ya faru katika makazi yao ya asili
Aidha, Mhe.Kanyasu amewataadhalisha watu wenye nia ovu wa kuhujumu faru hao hawatavumiliwa.
No comments:
Post a Comment