HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 12, 2019

JESHI LA POLISI KAGERA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi.
 Na Lydia Lugakila, Kagera

Jeshi la Polisi mkoani Kagera limejipanga kikamilifu katika kuhakikisha linatoa elimu ya uelewa kwa wananchi kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi pamoja na majanga yatokanayo na ajali za moto.


Kauli hiyo imetolewa Septemba 11, 2019 na Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Revocatus Malimi wakati akizungumza na vyombo vya habari katika ofisi za mkoa zilizopo katika manispaa ya Bukoba mkoani hapa.


Kamanda Malimi amesema jeshi hilo licha ya kuoa tahadhali mbalimbali lakini bado wananchi wamekuwa wagumu kuelewa athali zake hivyo wameamua kujipanga kikamilifu ili kuwafikia wananchi kwa lengo la kuoa elimu kupitia program maalum za falsafa ya polisi jamii ambayo itaweka umuhimu katika kuhakikisha vinafanyika vikao na wananchi vitakavyosaidia kusuluhisha matatizo kwa njia ya kuelimishwa kwa kuwatembelea wananchi popote waliopo.


Amesema Suala la kuelimisha jamii katika kuepukana na majanga mbali mbali ikiwemo kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, linahitaji ushirikiano mkubwa na taasisi mbali mbali kama za kiroho zinazotoa msaada wa kuhubiria amani,ili kuwakumbushaa wananchi kuachana na tabia hizo mara moja.


Pia Malimi amesema wanasiasa wanatakiwa watambue kuwa Wananchi ndio wafuasi wao hivyo ni wakati wa kutenga muda katika vikao vyao mbali mbali kuweka mkazo jambo jilo kama ajenda za kudumu na kuwakumbusha juu ya kutii sheria bila shuruti kila wanapokutana katika vikao vyao, kutafuta suruhu ya matatizo ya kwa njia ya mabaraza.

Ametaja kusikitishwa na baadhi ya wananchi wanachukua maamuzi magumu ikiwemo kujinyonga, mahuaji kwa watu wasio na hatia huku akitaja uwepo wa baadhi ya wananchi wanaofanya vitendo hivyo kwa kukusudia na kueleza kuwa matukio mengi ya kujinyonga husababishwa na watu kukata tama ya maisha, maradhi ya muda mrefu jambo ambalo si suruhu ya kumaliza matatizo hayo.



Hata hivyo amesema jeshi hilo linaendelea na mapambano Makali katika kuhakikisha vitendo vya magendo ya kahawa, wizi wa madini ,madawa ya kulevya uhamiaji haramu vinakomeshwa mara moja.

Aidha hivyo ametoa wito kwa wananchi kuacha mara moja kuyasogelea magari yanapopata ajali zitokanazo na ajali za moto.

No comments:

Post a Comment

Pages