HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 03, 2019

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA MIKOA

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, CGF Thobias Andengenye (pichani), amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Mikoa hapa nchini.

Makamanda walioguswa na mabadiliko hayo ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Zimamoto (SACF) Hamis Telemkeni, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Monitoring and Evaluation Makao Makuu Dodoma, anakwenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji (RFO) Mkoa wa Tanga.
 
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Zimamoto (SACF) Goodluck Urio, aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (RFO) Mkoa wa Tanga, anakwenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro.
 
Aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (RFO) Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Zimamoto (SACF) Ambwene Mwakibete, anakwenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto (ASF) Isabela Mbwago.

Vilevile Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto (ASF) Jumbe Kondo, anakwenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji (RFO) Mkoa wa Njombe.
 
Pia aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Zimamoto (ACF) Gilbert Mvungi, amehamishiwa Makao Makuu ya Zimamoto na Uokoaji Dodoma. 

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaendelea kutoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Makamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mikoa na Wilaya katika suala la Kinga na Tahadhari Dhidi ya majanga na maokozi.

No comments:

Post a Comment

Pages