HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 03, 2019

MASHEIKH KAGERA WAHIMIZA AMANI

Na Lydia  Lugakila, Kagera
 
Sheikh Twahili Ismail Tabilane (70) kutoka Kijiji cha Burembo Kata ya Mushasha wilayani Misenyi mkoani Kagera amerejea salama hapa nchini akitokea Makka Saudi Arabia katika kutekeleza ibada ya hijja ya dini ya kiislamu.
 Akizungumza akiwa nyumbani kwake katika hafla ya kumpongezwa kutoka katika ibada hiyo iliyofanyika Septemba 2,  2019, nyumbani kwake Burembo, wilayani Misenyi Mkoani Kagera.
Sheikh Ismail ambaye kwa sasa ni Khaji amesema kuwa kutokana na umoja  uliopo makka ikiwemo ushirikiano na upendo ni ishara kuwa kila muislamu aige na kujifunza na kutaja safari hiyo kuwa ya neema kubwa iliyosababisha yeye kurudi hapa nchini akiwa salama hivyo ametamani tena kurudi nchini makka.
Sheikh  huyo amesema kila muislamu aione  habari ya kwenda hija kama ya kawaida na kuwa kila muumini wa dini hiyo atekeleze suala la kufika makka.
‘’Namshukuru mungu hali niliyoikuta kule makka ni nzuri natamani kurudi mwaka ujao hii ni neema kule hakuna cha Tajiri wala maskini kule ni haki sawa kwa wote amesema’’
Amesema safari ya kwenda hijja  haina ubaguzi kwani  hija hiyo inawapa waislamu wote haki sawa, ikiwemo chakula cha bure, maradhi na  mahitaji mengineyo muhimu pamoja na kupewa mafunzo ikiwemo kusoma vitabu vya Quruan takatifu vyenye maudhui ya kuiheshimu dini hiyo.

Kwa upande wake sheikh mkuu wa mkoa wa kagera Sheikh Haruna Kichwabuta amewahimiza waislamu mkoani kagera kuendelea kuwa wamoja  na kumuomba mungu ili kila muumini wa dini hiyo aweze kufikia makka.
Hata hivyo shekhe Kichwabuta meyashukuru  madhehebu tofauti mkoani Kagera yaliyoshiriki kwa kumpokea shekhe Twail aliyekwenda kuwakilisha dhehebu hilo katika ibada hiyo.
Amewataka waislamu kujitokeza kwa wingi mwaka ujao 2020 kuudhulia ibada ya hijja

Naye Sheikh  Mkuu Wilaya ya Misenyi mkoani hapa, Sheikh Abduzaydi Kyagulani, ametoa pongezi kwa sheikh huyo kurejea salama hapa nchini  na kuhimiza umoja kwa waumini hao na madhehebu tofauti ikiwemo kuiombea nchi amani.
Amesema kuwa masheikh kutoka Kanyigo, Buyango, kilimilile, mtukula, Bugandika, Burembo wote wamelejea kwa usalama bila matatizo ambapo ameongeza kuwa madhumuni mazito ni kujenga nguzo tano za kiislamu sambamba na umoja.
 Sheikhe wa Mkoa wa Kagera, Sheikh Haruna Kichwabuta akimpongeza Shekhe Twahili aliyetoka Makka kuhiji.
 Hapo ni Sheikh wa Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Abduzayid Kyagulani.
Waumini.
Katibu Mwenezi CCM Mkoa wa Kagera, Hamimu Mahamudu.

No comments:

Post a Comment

Pages