HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 03, 2019

Magufuli, Museven kufungua kongamano la biashara, uwekezaji

NA SULEIMAN MSUYA

RAIS John Magufuli na Rais Yoweri Museven wa Uganda wanatarajiwa kufungua Kongamano la kwanza la Biashara na Uwekezaji kati ya nchi hizo mbili Septemba 7 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Profesa Joseph Bushweishaija kongamano hilo litashirikisha wadau mbalimbali wa sekta husika.

Taarifa hiyo ilisema kongamano hilo litashirikisha wazalishaji, wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.

"Septemba 6 Rais Magufuli na Museven watafungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji  ambalo litashirikisha wazalishaji, wafanyabiashara na wananchi wa nchi zote mbili," ilisema taarifa.

Aidha, taarifa hiyo ya Prof Bushwaishaija ilisema katika kongamano hilo kutakuwa na maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali kutoka Tanzania na Uganda.

Katibu mkuu amewataka Watanzania kutumia fursa kongamano hilo kama fursa ya kuonesha bidhaa za kilimo, viwandani na huduma zinazotolewa na taasisi za umma na binafsi.

"Ili kushiriki kongamano na maonesho mwananchi anatakiwa kujisajili katika anauni iliyopo kwenye tovuti ya wizara ambayo ni www.mit.go.tz," alisema.

Kongamano hilo la kwanza kati ya Tanzania na Uganda linakuja zikiwa zimepita wiki chache baada ya kufanyika kwa Jukwaa la Biashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini.

Jukwaa hilo ambalo lilifanyika mapema mwezi wa Agosti lilihudhuriwa na Rais Magufuli na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na wafanyabiashara wa nchi hizo.

Inaaminika kuwa kupitia makongamano na majukwaa hayo ambayo yamekuwa yakiandaliwa na wizara ya viwanda na biashara kwa lengo la kuchochea ukuaji wa biashara na uchumi wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages