Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Hashimu Murshid Ngeze.
Na Lydia Lugakila, Kagera
Wazazi na walezi mkoani Kagera
wametakiwa kuacha dhana potofu ya kuwavunja moyo watoto wao hasa wanafunzi
wanapokaribia kufanya mitihani ya taifa kwa kuwatamkia neno FANYA VIBAYA MTIHANI ILI UWEZE KUSHINDWA.
Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 3,
2019 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Murshid Hashimu Ngeze katika kuelekea kufanya
mitihani ya Taifa kwa wanafunzi wa shule ya msingi kote nchini
Ngeze amesema kuwa kitendo hicho cha
mzazi au mlezi kumtamkia mwanaye kuwa afanye vibaya mtihani ili ashindwe ni kikwazo kikubwa kinachokwamisha juhudi na doto za mtoto katika
kufikia malengo yake tarajiwa.
‘’Si vizuri mtoto usimvunje moyo mwache mtoto afanye vizuri njia ya jinsi mtoto
atasoma ni mungu anayejua sisi Halmashauri tupo tunajua ni jinsi gani mtoto
atapata Elimu amesema.’
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa baadhi
ya wazazi wamekuwa na tabia ya kutoongea na watoto wao hasa mabinti katika misingi
iliyo bora, hivyo amewahimza wazazi na walezi
kununua vifaa muhimu vya watoto ili kunufaika na Elimu bure iliyoko hapa nchini.
Amesema ni muhimu sana wazazi
na walezi kukaa na watoto wao wa kike kuwafundisha jema na baya ili waweze
kukua ki maadili.
Katika hatua nyingine Ngeze amekemea
tabia za baadhi ya waendesha pikipiki maarufu kama boda boda wanaowadanganya
wanafunzi kwa kuwarubuni kwa zawadi na
lifti, kuwa tabia hiyo sio nzuri ambapo tayari mikakati mbali mbali inafanyika
ili kupambana na vitendo hivyo ambavyo huwafanya wanafunzi kukatisha masomo kwa
kupata ujauzito na kushinddwa kufikia malengo yao.
Amewataka wanafunzi wilayani humo
kufanya mtihani wao vizuri unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo Septemba kumi na moja na kumi na mbili mwaka
huu bila kuwa na vikwazo vya kusingizia kufuata shule umbali mrefu kwani tayari
ujenzi wa shule unaendelea wilayani humo.
Aidha ametoa shukrani za dhati kwa
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Magufuli kwa kitendo cha
kuwaita ikulu watendaji wa kata kote nchini kwa lengo la kuzungumza nao kwa kuwapa maelekezo ya
kuijenga nchi.
Akigusia sualala maendeleo amesema
kuwa katika utawala wa Rais Magufuli vijiji 94 katika halmashauri hiyo kila
mwaka kijiji kimoja kitakuwa kinapata elfu 45 katika
uendeshaji wa maendeleo kwenye vijiji hivyo.
Ametaja hatua hiyo kuwa kubwa kuwa ni
kutokana na juhudi za Rais Magufuli na kudai kuwa halmashauri hiyo
haijawahi kugusa fedha za maendeleo na
kuziweka katika shughuli za kawaida.
Ikumbukwe kuwa Halmashauri hiyo ina
kata 29 vijiji 94 na katika vijiji vyote hivyo vina miradi mbali mbali
inayoendelea miradi hii ipo katika
makundi matatu ambayo ni miradi ya serikali kuu,miradi ambayo inatoa fedha
kutoka mapato ya ndani na miradi ambayo ni ya wahisani kwa ushirikiano na wananchi.
Mwenyekiti huyo amewataka wananchi kushiriki katika miradi mbali mbali ya kimaendeleo kwa ukamlifu na kuguswa na miradi hiyo ambapo hadi sasa ameitaja Halmashauri hiyo
kuwa katika hatua nzuri kwani miradi
mingi inaendelea kutekelezwa ambapo usimamizi wa fedha ni mzuri pia.
Hata hivyo amesema kuwa serikali hutumia fedha nyingi katika
miradi ya maendeleo kwa wananchi hivyo ni vema
miradi hiyo itunzwe na kuilindwa.
Na kuwataka wananchi kutoa taarifa mara moja pale wanapogundua au kubaini baadhi ya watu wanaohujumu miradi hiyo ili hatua
kali ichukuliwe.
Taarifa za ukaguzi mbali mbali
zimekuwa zikifanyika ikiwemo ya CAG au ukaguzi wa ndani hama wakaguzi
kutoka mkoani ambapo mara nyingi wamekuwa wakiikagua na pale ambapo wamekuwa
wakikuta mapungufuwamekuwa wakishauri.
No comments:
Post a Comment