HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 03, 2019

TIGO YAZINDUA HOME INTERNET ROUTER

Mkuu wa Bidhaa na Huduma kutoka Tigo, David Umoh (kushoto), akimkabidhi kifaa cha ‘Home Internet Router’ Mtangazaji wa Clouds Tv, Abdallah Kamelo, katika uzinduzi wa huduma ya kwanza na ya kipekee ya ‘Home Internet’ kutoka Tigo. Katikati ni Ofisa Mkuu wa Biashara, Tarik Boudiaf. (Na Mpiga Picha Wetu).

NA SULEIMAN MSUYA

KAMPUNI ya Tigo Tanzania imezindua bidhaa mpya itakajulikana kwa 'Home Internet By TIGO' kwa ajili ya matumizi ya mtandao majumbani.

Bidhaa hiyo mpya imezinduliwa jana jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa ambapo imetajwa kuwa na ubora wa kimataifa.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo Ofisa Biashara Mkuu wa Tigo, Tarik Boudiaf alisema bidhaa hiyo ni moja ya bidhaa bora katika matumizi ya mtandao katika familia.

Alisema bidhaa hiyo imetengenezwa kwa ubunifu wa hali ya juu ili kuhakikisha jamii ya Kitanzania hasa wanafamilia wananufaika nayo.

"Leo tumezindua huduma mpya ya " Home Internet By TIGO' ambayo ni ya kwanza hapa nchini lakini pia huo ni mwendelezo wa Tigo kuja na huduma bora za kisasa,"alisema.

Boudiaf alisema Tigo imekuwa ya kwanza kuja na bidhaa ya Tigo Pesa App, kuwezesha kutuma fedha nje ya nchi na nyingine nyingi.

Mkuu wa Bidhaa na Huduma Tigo, David Umoh alisema bidhaa hiyo inarahisisha mambo mengi kwa mtumiaji wa mtandao.

Alisema kupitia bidhaa hiyo mteja ataweza kuangalia salio, dakika, muda aliotumia na kuongeza salio bila kutoa laini ya simu.

Meneja Vifaa wa Tigo, Mkumbo Mnyonga alisema bidhaa ya 'Home Internet By TIGO' itakuwa inapatikana kupitia Tigo App hivyo kuwaomba watumiaji wa mtandao huo kupakua App hiyo.

Alisema bidhaa hiyo inaruhusu kutumiwa zaidi ya vifaa au watu 32 kwa wakati mmoja hivyo itarahisisha huduma ya mtandao katika familia.

"Hii ni zaidi ya mtandao naamini watumiaji watanufaika zaidi kwani ule utaratibu wa watu kutoa laini ya simu ili kuunga kifurushi umefikia kikomo," alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages