Ofisa Mkuu wa Tigo Business, Pavan Ramdhani, akimkabidhi kifaa cha 'Routers' Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la TanzaniaDaima, Suleiman Msuya aliyeshinda bahati nasibu, baada ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ (Picha na Mpiga Picha Wetu).
NA SULEIMAN MSUYA
KAMPUNI ya simu ya
Tigo, kupitia kitengo chake cha Tigo Business imezinduzi huduma mpya ya ‘Office
Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini.
Afisa Mkuu wa Tigo
Business, Pavan Ramdhani, aliwaambia waandishi na wateja wa Tigo kuwa, kuwa
huduma hiyo ni ya kisasa na inaenda na wakati na imeshirikisha wataalamu wa
Microsoft.
Ramdhani alisema huduma
hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft hivyo kuifanya Tigo
kuendelea kuwa kinara wa ubunifu na kuiwezesha kufanya biashara zake kwa
malengo.
“Sambamba na uzinduzi
wa huduma ya ‘Home Internet’ uliyofanywa
na Tigo hivi karibuni, huduma ya ‘Office
Internet’ inakuja na faida endelevu kwa wateja wenye biashara ndogo na za kati
ambao hupendelea huduma za intaneti kwa mkataba. Hii inadhihirisha matumzi bora
ya mtandao wa wenye kasi nchini Tanzania wa 4G+.
“Tulifanya kazi kwa
ushirikiano wa karibu sana na wateja wetu, ambapo walituonyesha maeneo matatu
muhimu yenye changamoto; Muda unaotumika kuunganisha huduma ya intaneti, Kasi
ya huduma hiyo na ukosefu wa maana halisi,
Matumizi ya intaneti na zana zenye uhusiano na biashara,” alisema.
Kwa upande wake Kaimu
Mkuu Mauzo Tigo, Niki Kazuka wana furaha kutangaza huduma hiyo ya aina yake
hapa nchini na kuwaomba wafanyabiashara wadogo na kati kuitumia kibiashara.
“Office Internet ina
huduma ya daraja la kwanza iliyounganishwa na mtandao wa Tigo 4G+, wenye watumiaji wengi duniani kote chini ya
ushirikiano wa Microsoft,” alisema.
Alisema huduma hiyo inatumika
bila muunganisho wa waya, kwa maana ya kwamba mteja wao anatakiwa kuwasha kifaa
chake cha Modem au Router.
Mtaalam wa Biadhaa
Kitengo cha Tigo Business, Brayan Swai alisema kifaa hicho kina uwezo wa
kuunganisha vifaa 10 hadi 32 kwenye inteneti kwa mara moja.
“Microsoft 365
inaruhusu kufanya mambo mbalimbali ikiwamo utumaji wa barua pepe za
kibiashara, kutuma na kuhifadhi ujumbe
katika mtandao, matumizi ya Microsoft katika masuala yote ya kibiashara ikiwamo
mikutano ya moja kwa moja mtandaoni,” alisema.
No comments:
Post a Comment