HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 13, 2019

Waandishi wengi hawaiju sheria inayowasimamia

Mkurugenzi wa Tamwa, Rose Ruben, akichangia mada kwenye mkutano huo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam shule ya Uandishi wa Habari na mawasiliano ya umma, Abdallah  Katunzi akizungumza jambo wakati wa mkutano huo.
Saum Mwalimu kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) akizungumza kwenye mkutano huo kuhusu namna Baraza hilo linavyotoa utetezi na elimu kuhusu sheria ya habari ya mwaka 2016.


NA MWANDISHI WETU

WADAU wa habari nchini wamesema waandishi wengi wa habari hawaijui sheria inayowasimamia hali inayowaweka kwenye hatari ya kuivunja sheria hiyo.

Wakizungumza wakati wa mkutano wa siku moja ulijadili maadili kwenye vyumba vya habari, ulioandaliwa na Shirika la Internews chini ya mradi wa Boresha Habari, walisema lazima nguvu iongezwe ili wanahabari waifahamu na kuisimamia sheria hiyo vizuri.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Shule ya Uandishi wa Habari na Mwasiliano ya Umma, Abdallah Katunzi alisema maadili ni tatizo kubwa kwa wanatasnia ya habari.

"Kuna tafiti tulifanya mwaka jana tukaangalia habari zinazotuhumu tukagundua asilimia 50 ya habari hizo waliotuhumiwa hawakupewa nafasi ya kujieleza. Sasa kama wote hao wakienda mahakamani media zitakuwa kwenye wakati mgumu.

"Vyumba vingi vya habari havina maadili mwaka jana tulifanya utafiti kuhusu maadili na masuala ya fedha kwenye media houses 25 tulichokikuta huko ni majanga.

"Mwaka huu tutafanya tena utafiti huo kwenye media hoses 30 nchi nzima lengo ni kuona ukubwa wa tatizo na kutafuta namna sahihi zaidi kukabiliana nalo," alisema Katunzi.

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Rose Ruben aliitaka jamii kuelewa sio kila mtu anaweza kuwa mwandiahi wa habari.

"Ufike wakati na sisi waandishi wa habari tuwe na mchujo kama ilivyo kwa wanasheria, tuache kulalamika na jamii ujue sio kila mtu ni mwandishi wa habari hata kama anaweza kupiga picha na kuandika maelezo ya picha," alisisitiza.

Mhadhiri Mary Kafyome kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam, alisema suala la maadili linaanzia kwenye ngazi ya familia hivyo wazazi lazima watimize wajibu wao.

"Unakutana na mwanafunzi wa Chuo Kikuu unajiuliza alipitaje huko kwingine... yaani msingi wake sio bora kabisa hajiwezi hama nidhamu.

"...Tunakutana nao huko ila sio wote wapo wachache wanajiewa unaona uwezo wao wanavyojituma unafutahi," alisema Kafyome.

Mshauri wa masuala ya habari na Mhariri Mwandamizi, Jesse Kwayu alisema kuyumba kwa uchumi wa nchi kumesababisha kujaribika kwa maadili kwenye vyumba vya habari.

"Wahariri wana hofu kwanza ya kukosa matangazo yanayowapa hela za kujiendesha hivyo ipo nguvu inayoshuka kwao na kuwafanya wasiandike aina ya habari.

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Internews, Wenceslaus Mushi, alisema ni muda wa wadau kuja na suluhisho la tatizo hilo wakishirikiana na serikali huku akiahidi kuendelea kufanya mikutano ya aina hiyo ikiwashirikisha maofisa wa serikali wenye dhamana ya habari.

No comments:

Post a Comment

Pages