Baadhi ya wafanyabiashara wakifurahia jambo wakati wa Kongamano la Wanachama wa Klabu ya Wafanyabiashara Mkoa wa Tabora uliolenga kuwapa mafunzo na nidhamu ya biashara. Kongamano hilo liliandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya kuwapa elimu na fursa za kukuza biashara zao kupitia benki hiyo. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu, Tabora
Wafanyabiashara katika Mkoa wa Tabora, wengi
hawajilipi mishahara kutokana na kazi zao wanazofanya na hivyo kukosa fursa
ya kufahamu namna biashara zao zinavyokua au zinavyodorora.
Haya yamebainishwa na Meneja wa NMB kanda ya
Magharibi, Sospeter Magese,wakati akizungumza na wafanyabiahara wa Mkoa wa
Tabora, alisema wengi huwa hawajilipi
mishahara na kufanya mahesabu yao kutokuwa vizuri.
“Inashangaza mfanyabiashara anawalipa wafanyakazi
wake mshahara lakini yeye akiwa mkurugenzi hajilipi mshahara na pia huchanganya matumizi binafsi na ya biashara jambo amvalo huyumbisha mitaji yao.
Akizungumza katika kikao cha kupokea maoni ya
wafanyabiashara juu ya huduma inayotolewa na NMB, Magese aliwaeleza kuwa kupitia
mishahara yao ndio matumizi ya binafsi yanaweza kutoka huko na sio katika
biashara.
Aliwaeleza kuwa benki ya NMB ni benki yao na waitume
kwani imejipanga kushirikiana nao katika kukuza uchumi wa Taifa.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wenye akaunti benki ya
NMB,Ahadi Mviombo,aliwahimiza wafanyabiashara kutenga sehemu ya mauzo yao kwa
ajili ya kulipa madeni wanayokopa.
“Kama ukiweza kutenga angalau shilingi elfu tano
kila siku kwa ajili ya marejesho mtihani utakuwa umeshinda”Alisema
Mfanyabiashara Mwalimu Mambo,aliipongeza NMB kwa
utaratibu wake wa kuwafundisha wafanyabiashara namna ya kuweka mahesabu sawana
kutafuta faida.
“Tunashukuru kwa elimu tunayopewa na benki hii
ambayo kwa kweli inatusaidia sana katika biashara zetu”Alisema
Kikao hicho chenye lengo la kupokea maoni kutoka kwa
wafanyabiashara ziadi ya 300 wenye akaunti NMB pia kilihudhuriwa na wafanyakazi wa benki hiyo
ambao walitoa elimu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.
No comments:
Post a Comment