Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen, mkutano huo umefanyika Mjini Bet Dagan 50250 nchini Israel tarehe 5 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za wizara hiyo eneo la Bet Dagan 50250 nchini Israel, tarehe 5 Septemba 2019.
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za wizara hiyo eneo la Bet Dagan 50250 nchini Israel, tarehe 5 Septemba 2019.
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za wizara hiyo eneo la Bet Dagan 50250 nchini Israel, tarehe 5 Septemba 2019.
Na
Mathias Canal, Bet Dagan-Israel
Waziri
wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) tarehe 5 Septemba 2019 amekutana
na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe
Uri Yehuda Ariel HaCohen na kukubaliana kwa kauli moja kuwa serikali za nchi
hizo mbili kuingia makubaliano ya kuendeleza kilimo hususani katika utafiti,
Tija katika uzalishaji, na Teknolojia.
Katika
mkutano huo uliohudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud
Masima, Mhe Hasunga ametoa shukrani kwa Serikali ya Israeli kuipatia Tanzania
nafasi 100 za kujifunza kuhusu sekta ya kilimo kwa vijana kupitia programu
inayosimamiwa na Agrostudies.
Waziri
Hasunga ameeleza katika mkutano huo dhamira ya Serikali ya Tanzania inayoongoza
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli, ya kuwasaidia
vijana waliorudi nyumbani baada ya mafunzo hayo kwa kuanza kuwapatia mahitaji
ya msingi ikiwemo ardhi ambayo ipo eneo litakalowawezesha kujiendeleza.
Vilevile
ameeleza kuwa katika wizara ya kilimo hakukuwa na kitengo cha masoko hivyo ili kuwaunganisha
vijana hao na masoko ya biashara watakazozalisha serikali ya Tanzania kupitia
wizara ya Kilimo imeanzisha kitengo maalumu cha kushughulikia masoko ya mazao mbalimbali
ya wakulima.
Waziri
Hasunga pia amezungumzia kuhusu maeneo yanayoweza kuwavutia wawekezaji kutoka Israeli
ili kuwekeza nchini Tanzania kwa kutoa takwimu za ukubwa wa ardhi yenye rutuba,
uwepo wa maji na hali ya hewa inayoruhusu ukuaji wa aina nyingi ya mazao.
Serikali
ya Israeli ipo tayari kusaini hati ya makubaliano ya kilimo (Memorandum Of Undarstanding-MOU)
ya kilimo pale itapowasilishwa na Serikali ya Tanzania, hii imekuja baada ya
Mheshimiwa Waziri Hasunga kuona umuhimu wa kuingia makubaliano ili iwe rahisi
wawekezaji kutoka Israel kuzuru Tanzania kuwekeza pamoja na kupata mikopo
kutoka katika Serikali yao.
Akizungumza
kwa niaba ya Serikali ya Israeli Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa nchi
hiyo Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen imehaidi pindi Serikali ya Tanzania
itakapowasilisha mahitaji hasa kwenye mazao ambayo muhimu ya kuanza nayo kwa
ajili ya soko la Israel itakuwa tayari kushirikiana kwa kutoa ujuzi pamoja na
uwezeshaji wa wataalamu.
Hata
hivyo itakapotokea mwekezaji wa Israeli ataposhirikiana na kampuni ya Tanzania,
Serikali inawajibu kuingilia kati kusaidia maeneo ya uwezeshaji na rasilimali
watu.
No comments:
Post a Comment