HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 07, 2019

WAZAZI WATAKIWA KUKEMEA MIMBA ZA UTOTONI

Katibu  wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa wa Kagera, Angelus Kamgisha, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera. (Picha na Lydia Lugakila). 


Na Lydia Lugakila

Wazazi walezi na wananchi  mkoani Kagera wametakiwa  kukemea na kutoa taarifa mara wanapoona au kuhisi kuwepo kwa vitendo vya baadhi ya watu wanaowapa mimba watoto na kusababisha kukatisha  masomo na ndoto zao.

Kauli hiyo imetolewa Septemba 6, 2019 na Katibu  wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa wa Kagera, Angelus Kamgisha, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM zilizopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Kamgisha akitoa wito kwa wazazi walezi na wananchi kukemea tatizo hili la  mimba za utotoni zinazosabaisha kukatisha masomo na ndoto zao ametaja  vitendo hivyo kuwa kero licha ya kupigiwa kelele kila mara na baadhi ya viongozi.

Amesema elimu bure imetolewa hapa nchini kwa ajili ya kumpatia uelewa mtoto lakini baadhi ya watu wasiojua misingi,sheria na kanuni za nchi wameendele kukiuka utaratibu katika kufanya vitendo hivyo ambavyo ulifedheesha taifa kutokana na kuwakosa wategemewa wa baadae.

‘’Watoto hukatishwa masomo, ukaa majumbani kwa sababu ya kupewa ujauzito huku wengine wakiwa bado katika umri mdogo changamoto kubwa ipo kwa wazazi kutotoa ushirikiano wa kutoa taarifa sahihi pale binti anapata ujauzito matokeo yake inamhathiri kisaikolojia huyo binti,’’amesema.

Katibu huyo amesema wazazi wanapaswa kushirikiana na vyombo vya dora kwani hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati anaingia madarakani alisisitiza jambo hilo hivyo ni vema wazazi wawahimize watoto wao kwenda shule.

Sambamba na hayo amewataka vijana kuachana na makundi mabovu ya mmomonyoko wa maadili, huku akiwataja waendesha pikipiki kuwa chanzo cha kuharibu watoto wa shule kuacha tabia hizo mara moja.

Amesema  waendesha pikipiki wameeongelewa sana katika baadhi ya sehemu tofauti kutokana na kuwa kikwazo kwa kuwarubuni watoto wa shule kwa rifti zinazojenga vishawishi vya kuwapa mimba wanafuzi ambpo amewataka kuacha tabia hiyo mara moja.

Amesema juhudi kubwa za serikali ni kuwa na mpango wa kuhimiza kujengwa kwa mabweni shuleni ili kuepukana na watoto wa kike kuembea umbari mrefu ambapo tayari kila kata ina shule ikilinganishwa na awali.

Hata hivyo amesema katika  barazaa la Jumuiya ya wazazi la mkoa limetolewa azimio kuwa kila wilaya iunde kamati ya kutoa elimu juu ya maadili mema kwa vijana walioko mashuleni na  mitaani, kufuatilia afya na mazingira ambapo tayari kamati hiyo imeanza kuzaa matunda katika wilaya ya Ngara mkoani hapa.

No comments:

Post a Comment

Pages