WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amezielekeza mamlaka husika ziwachukulie hatua za
kinidhamu watu wote ambao hawakutekeleza majukumu yao ipasavyo kufuatia
tukio la ajali ya moto iliyotokea Agosti 11, 2019 mkoani Morogoro na
kusababisha vifo vya watu 104, majeruhi pamoja na uharibifu wa mali.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Septemba 13, 2019) , wakati akiahirisha mkutano wa 16 wa Bunge la 11, Bungeni jijini Dodoma. Bunge limeahirishwa hadi tarehe 3, Novemba mwaka huu.
“Baada ya tukio hilo la kusikitisha tarehe 12 Agosti 2019niliunda
Kamati Maalumu kwa lengo la kufanya uchunguzi wa kina kuhusu ajali hiyo
iliyosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.”
“Lengo
lilikuwa kufahamu chanzo cha ajali, mazingira baada ya ajali na hatua
gani zichukuliwe kuzuia matukio kama haya sambamba na kuwawajibisha wale
wote ambao hawakutekeleza wajibu wao ipasavyo kabla na baada ya ajali
kutokea.”
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwashukurumadaktari na wahudumu wa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili nawadau wote ambao walishiriki kuokoa maisha ya waathirika wa ajali hiyo tangu ilipotokea.
“Nawasihi Watanzania wenzangu tujifunze kutokana na ajali hiyo iliyotokea Morogoro na hivyo kuepuka mikusanyiko
ya aina hiyo katika maeneo ya ajali. Aidha, tujenge nyoyo za huruma na
kuwa wepesi wa kutoa msaada kwa waathirika wa ajali badala ya kutumia
kama fursa za kujinufaisha isivyo halali.”
No comments:
Post a Comment