Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti, akizungumza na wawekezaji katika seka ya ufugaji kutoka Rwanda ofisini kwake.
Na Lydia Lugakila, Bukoba
Wawekezaji kutoka nchi jirani sasa
wapishana kuchangamkia uwekezaji kagera ni baada ya wiki ya uwekezaji
kuwaonesha fursa.
Juhudi za viongozi wa Mkoa wa Kagera kuufanya mkoa huo kuwa
kitovu cha uchumi wa nchi za Afrika Mashariki na Kati zilizoanzia katika Wiki
ya Uwekezaji Kagera sasa zaanza kuzaa matunda ni baada ya kundi la wawekezaji
kutoka nchi jirani ya Rwanda kuitikia wito wa kuwekeza mkoani humo.
Kundi hilo la Wawekezaji wapatao kumi ambao ni wamiliki wa makampuni
mbalimbali ya biashara nchini Rwanda walioamua kuunda Kampuni moja ya uwekezaji
mkoani Kagera katika Sekta ya ufugaji wa kisasa na kuanzisha kiwanda cha
kusindika nyama wamewasili moani hapa Septemba 11 mwaka huu katika ofisini ya
Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ili kumweleza nia yao na kuwa
wapo tayari kuwekeza katika ufugaji na kiwanda cha kusindika nyama.
William Kawamala ni kiongozi
wa wawekezaji hao kumi kutoka nchini Rwanda amemweleza Mkuu wa Mkoa Gaguti kuwa
wapo tayari kuwekeza katika sekta ya ufugaji
wa kisasa wa ng’ombe katika Kampuni za
Ranchi za Taifa (NARCO) baada ya kupata fursa hiyo katika Wiki ya
Uwekezaji Kagera iliyofanyika tarehe 12 hadi 17 Agosti, 2019.
“Sisi baada ya kushiriki Wiki ya Uwekezaji Kagera tulivutiwa
kuwekeza katika Sekta ya ufugaji, na tuliporudi kwetu nchini Rwanda tulikaa
pamoja na kukubaliana tujiunge kwa pamoja wafanyabiashara kumi ili kuanza
uwekezaji mara moja, ndiyo maana tupo hapa ili kuanza hatua za awali pia tumekuja
kuona maeneo ya kufugia na kuweka kiwanda..”
Amefafanua Kawamala’’.
Mkuu wa Mkoa Gaguti amewakaribisha wawekezaji hao na kusema
kuwa mkoa upo tayari kuwapa ushirikiano, hatua ya kwanza amemwelekeza Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa NARCO Prof. Philemon Wambula pamoja na baadhi ya wataalam kutoka
Sekretarieti ya mkoa kuwaonesha maeneo
yaliyotengwa ili wakubaliane nayo na taratibu za kusajili kampuni na kuanza uwekezaji zianze
mara moja.
“Baada ya Wiki ya Uwekezaji mwitikio umekuwa mkubwa sana wa
wawekezaji kuja kwetu kuchangamkia fursa zilizopo Kagera na sisi tumejipanga
tunawapokea na kuwaelekeza taratibu za uwekezaji, lakini jukumu letu ni
kuhakikisha fursa zote ambazo wawekezaji wameziona wanazitumia katika uwekezaji
ili kukuza uchumi wa mkoa wetu.” Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti.
Profesa Philemon Wambula Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni za
Ranchi za Taifa (NARCO) alisema kuwa mkoa wa Kagera bado una fursa kubwa za
uwekezaji katika sekta ya mifugo hasa katika viwanda vya kusindika nyama na
maziwa pia uwekezaji katika malisho ya mifugo aidha, NARCO bado inayo maeneo
makubwa ya kuwekeza.
Wawekezaji hao kumi walieleza kuwa baada ya kuona maeneo
wanataka kuwekeza katika ufugaji wa kisasa wa ng’ombe, ujenzi wa kiwanda cha
kuchinja na kusindika nyama kwa viwango vya kimataifa.
“Kwasasa baadhi ya Hoteli
kubwa nchini Rwanda zimeanza kuagiza nyama kutoka nchi za Ulaya wakati tukifuga
kisasa hapa Kagera tunaweza kuilisha Rwanda.” walisisitiza Wawekezaji hao kutoka nchini Rwanda.
No comments:
Post a Comment