HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 10, 2019

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA MKOA DODOMA, NA MZAKWE MAKUTOPORA


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, akimsikiliza mtoto Ernest Michael (6) mkazi wa Nkuhungu Dodoma aliyelazwa katika Hospitali ya Mkoa Dodoma kwa matibabu wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kuangalia changamoto mbalimbali zilizopo kwenye hospitali hiyo. Kulia ni baba wa mtoto huyo, Michael Yohana. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).



Na Mwandisi Wetu


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,amemuagiza Meneja Msaidizi wa Usimamizi wa Rasilimali za Misitu TFS Kanda ya kati Dodoma Bibi Tebby Yoramu kufuatilia Utafiti wa Udongo kwenye eneo la Mzakwe Makutopora Jijini Dodoma.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati alipofanya Ziara ya kushtukiza kuona maendeleo ya ukuaji wa Miti ya aina mbalimbali iliyopandwa katika eneo lindwa la Hifadhi ya Chanzo cha Maji linalotunzwa na Jeshi la kujenda Taifa JKT Makutopora ambapo amesema kuwa azma ya kuifanya Dodoma kuwa ya Kijani ipo pale pale.

Makamu wa Rais ameupongeza uongozi wa Kambi ya Jeshi ya Makutupora, Wakala wa Misitu Tanzania na Watendaji wa Ofisi yake kwa kuhakikisha miti iliyopandwa mwezi Desemba 2017 inastawi Vizuri.

“Vitabu vya dini vinasema Moja kati ya sadaka endelevu ni kupanda miti, miti hii imekuwa na kustawi kwasababu ya jitihada zenu za kuimwagilia na kuitunza, msikate tamaa, endeleeni na kazi hii njema ambayo matokeo yake yanaonekana ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa mifumo ya hali ya hewa ambayo huimarisha shughuli za kilimo na maendeleo ya viwanda.” Alisisitiza Makamu wa Rais

Nae Mkuu wa Kambi ya Jeshi ya Makutupora Luteni Kanali Festo Mbanga amesema kuwa miti 2300 ilipandwa tarehe 21/12/2017 na kati ya hiyo miti 2076 imekuwa na kustawi ikiwa ni sawa na asilimia 90.3 ya miti yote iliyopandwa.

“Katika miti iliyooteshwa awali baadhi haikuota, hivyo tumefanya jitihada za kuirudishia, tumepanda takriban miti 300 ya ziada” alisema Luteni Kanali Mbanga.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameagiza Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kuhakikisha tafiti zinakamilika mapema kutoka katika sampuli ya udongo iliyochukuliwa ili kubaini aina ya miti inayostawi katika eneo hilo na Jiji la Dodoma kwa Ujumla.

Kampeni ya Kukijanisha Dodoma ilizinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 21/12/2017 katika eneo la Mzakwe Jijini Dodoma ambapo miti 2300 ilipandwa siku hiyo.

Hayo yamesemwa leo mara baada ya kutembelea shamba la miti lililopo katika eneo la Mzakwe katika Kambi ya Jeshi la Makutupora Jijini Dodoma, ikiwa ni ufuatiliaji wa Kampeni aliyozindua mwaka 2017 ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.

Wakati huo huo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya Ziara ya Kushtukiza katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma kuangalia Changamoto mbalimbali ziliopo kwenye Hospitali hiyo, na kuagiza Uongozi wa Hospitali hiyo kushuhulikia na kusimamia vizuri matumizi ya fedha kwa ajili ya mahitaji yaliyopangwa.

No comments:

Post a Comment

Pages